HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAANDAMANO YA KUPINGA UJANGILI WA TEMBO NCHINI YAFANYIKA JIJINI DAR


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana pamoja na waandamanaji wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ mara baada ya kuwapokea leo, Ubungo  jijini Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (aliyeshika karatasi nyeupe mstari wa mbele) akiwa ameungana na msafara wa waandamanaji eneo la Ubungo kutembea nao hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo atapokea risala kutoka kwa waandamanaji.
 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
Matembezi hayo ya kupinga ujangili yameandaliwa Bw. Patric Patel, Mkurugenzi, African Wildlife Trust (wanne kutoka kulia msitari wa mbele) yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi na Ulimwengu mzima kwa ujumla juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha raia wa nchi mbalimbali duniani.

Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo ametoa wito kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona; na taasisi zote za umma zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.

HABARI NA MICHUZI BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: