Mshambuliaji wa Simba, Hamis Tambwe (kulia)
akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mafunzo, Jumbe Omari Jumbe katika mchezo wa
kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hekaheka katika lango la Mafunzo.
Beki wa Mafunzo Ali Vuai Juma (kushoto)
akichuana na mshambuliaji mpya wa Simba kutoka Burundi, Hamis Tambwe katika
mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.(Picha na Francis Dande)
Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini
Beki wa Mafunzo, Jumbe Omar Jumbe akimdhibiti mshambuliaji
wa Simba, Hamis Tambwe.
Golikipa wa timu ya Mafunzo ya Unguja, Ussi Makame Ussi akiwa
hana la kufanya baada ya kushindwa kuzuia kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa
Simba, Hamis Tambwe (kushoto) na kuipatia
timu yake bao la kwanza katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Golikipa wa Mafunzo, Ussi Makame Ussi akiruka
bila mafanikio kujaribu kuokoa mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Simba, Hamis
Tambwe na kuhesabu bao la
kwanza kwa timu yake.
Hamis Tambwe akishangilia bao aliloifungia timu yake.
No comments:
Post a Comment