Wapiganaji
wa Jeshi la Wananachi wa Tanzania { JWTZ } wakitoa salamu zao za mwisho
wakati wa mazishi ya kamanda wao Meja Khatibu Shaaban Mshindo
yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani. Meja
Khatib Shaaban ambae alikuwa Mkuu wa Kambi ya Kibaha alifariki dunia
Mjini Goma Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo akiwa katika ulizi wa amani
katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiongoza mamia ya wanajeshi,
wananchi na Ndugu na jamaa katika Mazishi ya Meja wa Kikosi cha JWTZ
Khatib Shaaban Mshindo, aliyeuawa Nchini DRC akiwa katika shughuli za
ulinzi wa vikosivya Umoja wa Mtaifa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud
Mohammed akitia udongo kwenye kaburi wakati wa mazinshi ya Meja Khatibu
Shaaban Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Mwakilishi
wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa vilivyopo Mjini Goma Nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo Meja E.B. Samuel akitia udongo kuashiria ushiriki
wa Umoja wa Mataifa katika mazishi ya Marehemu Meja Khatibu Shaaban
Mshindo yaliyofanyika kijijini kwake Mangapwani.
Mamia
ya wananachi, ndugu na Jamaa walioshiriki kuusitiri mwili ma marehemu
Meja Khatibu Shaaban katika mahali pake Huko Mwangapwani Wilaya ya
Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Kiongozi wa
Familia ya Marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo bwana Alhaji Machano
Mtumweni mara baada ya kukamilika kwa mazishi ya Kamanda huyo
yaliyofanyika kijiji kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Meja Khatibu Shaaban Mshindo aliyefariki Dunia akiwa katika shughuli za ulinzi wa amani katika kikosi cha umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo amezikwa kwa heshima zote za Kijeshi.
Meja
Shaaban ambaye alijeruhiwa vibaya kwa bomu katika eneo lake la kazi na
kusababisha kuvuja damu nyingi na hatimae kusababisha kifo chake akiwa
njiani kupelekwa Hospitali alizikwa kijiji kwao Mangapwani Wilaya ya
Kaskazini B, Mkoa Kaskazini Unguja.
Makamanda
na wapiganaji wa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania , askari wengine wa
vikosi vya ulinzi, wananchi , ndugu wa marehemu walishiriki kwenye
mazishi hayo wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed.
Marehemu
Meja Khatib Shaaban Mshindo alizaliwa Tarehe 29 Septemba 1972 katika
Mtaa wa Rahaleo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi na baadaye
kupata elimu yake ya msingi na kuhitimu mwaka 1986.
Alijiunga
na Skuli ya Sekondari uchama na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1990
ambapo baadaye akajiunga na kidato cha tano na sita katika skuli ya
sekondari ya Alharamain na kumaliza mwaka 1993.
Meja
Khatib Shaaban Mshindo alijiunga na Jeshi la wananchi wa
Tanzania { JWTZ } Tarehe 1 machi 1995 na kutunukiwa heshima
ya kamisheni tarehe 17 mei 1997.
Katika
utumishi wake Meja Khatib Shaaban Mshindo alibahatika kuhudhuria
mafunzo ya afisa mwanafunzi chuoni Monduli, kozi ya uongozi wa platuni,
uongozi wa kombania pamoja na mafunzo ya operesheni Nchini Canada mwaka
2008.
Kamanda
Khatib kutokana na ukakamavu wake alipandishwa vyeo kuanzia nafasi ya
Luteni mwaka 1998, kepteni mwaka 2004 na kufikia cheo cha meja mwaka
2010 wadhifa aliokuwa nao hadi kufariki kwake.
Marehemu
Meja Khatibu Shaaban Mshindo aliwahi kushika madaraka ya Kamanda wa
Kikosi mwaka 1997, Mkufunzi kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2006 pamoja
na kuwa kamanda wa kombania Mkoani Kibaha.
Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua na kuthamini
mchango wa Meja Khatibu Shaaban Mshindo alimtunuku nishani ya Miaka 40
ya JWTZ.
Umoja
wa Mataifa katika mazishi hayo uliwakilishwa na Kamanda wa Vikosi vya
Umoja huo Mjini Goma Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Meja D.B
Samujeli .
Kamanda
Khatibu Shaaban Mshindo aliyelitumikia jeshi la Wananchi wa Tanzania
katika kipindi cha miaka 18 miezi saba na siku 28 ameacha kizuka mmoja
na watoto watatu.
Mwenyezi Muungu alilaze roho ya marehemu Meja Khatibu Shaaban Mshindo mahali peMa peponi. Amin.
No comments:
Post a Comment