HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MKUU WA MAJESHI TANZANIA DAVIS A. MWAMUNYANGE AWAVISHA NISHA MAOFISA WA JESHI KWA UTUMISHI BORA NA WA MUDA MREFU TANZANIA.

Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis A. Mwamunyange, akiwasili katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai, akiwa na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, tayari kwa kuwavisha Nishani Maofisa ya Jeshi Tanzania kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu  wa Majeshi Tanzania Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete. sherehe hizo zimehudhuriwa na Familia za Maofisa hao na Wananchi.  
Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis A.Mwamunyange akipokea bwaride maalum liloandaliwa katika sherehe hizo za kutowa Nishani kwa Maofisa ya JWTZ katika viwanja vya Kambi ya Jesji Iddi Bavuai Migombani Zanzibar.
Wapiganaji wa JWTZ wakipita mbele ya Mgeni Rasmini wa sherehe za kuwatunukia Nishani  Maofisa wa JWTZ , katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai Migombani Zanzibar.
 Endelea kutizama tukio hili kwa kubofya hapa chini

MKUU wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania LT COL M.K.Saburi. kwa niaba ya Amiri, Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Bavuai Zanzibar
MKUU wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania Meja II.Iddi, kwa niaba ya Amiri, Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Bavuai Zanzibar
MKUU wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema Tanzania Staf Sajeti Saida Mohammed,kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Bavuai Migombani Zanzibar.
Wananchi na Wanafamilia wakihudhuria sherehe za kuvishwa Nishani ya Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Maosisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania.

Wageni waalikwa katika sherehe za kuwavisha Nishani ya Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya kambi ya Iddi Bavuai migombani Zanzibar.
Maafande wa JWTZ wakiwa na furaha baada ya kuvalishwa Nishani ya Utumishi Bora nawa Muda Mrefu Tanzania katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai Migombani Zanzibar.


Mkuu wa Majeshi Tanzania Devis A.Mwamunyange akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Wananchi waliotunikiwa Nishani ya Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Tanzania, sherehe iliofanyika katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai Migombani Zanzibar. 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: