

Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo kama wananchi wengine akitoka ndani ya msikiti wa manyema barabara ya saba alipoenda kushuhudia Madhara yaliyosababishwa na Short ya umeme baada ya moto mkubwa kulipuka msikitini hapo.
Mtoto anasoma madrasa katika msikiti wa Manyema Barabara ya saba Dodoma akiangali baadhi ya vitu vilivyoungua baada ya mto mkubwa kuzuka Msikitini hapo jana mchana.(Picha na John Banda, Dodoma)
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waumini wa Msikiti huo wakisukuma maji yaliyotumika kuzima moto uliokuwa umeshika katika msikiti huo baada ya Hitilafu ya umeme na kusababisha hasara kubwa.
Waumini wa Msikiti wa Manyema uliopo Barabara ya Saba Dodoma wakiangalia mabaki ya samani za msikiti huo ulioshika moto ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa hitilafu ya umeme.
Wakitoa madhuria yanayotumiwa
katika swala mbalimbali na waumini wa msitiki wa Manyema baada ya
kuunguzwa na moto uliosababishwa na Hitilafu ya umeme.
Na John Banda, Dodoma
MOTO mkubwa umezuka katika msikiti wa manyema uliopo
barabara ya saba manispaa ya Dodoma na kusababisha uaharibifu wa sehemu ya jingo
hilo pamoja na samani mbalimbali.
Mashuhuda wa Tukio hilo waliliambia jamb oleo kuwa baada
ya kuswali swala ya ijumaa na kuondoka walishtukia moshi mkubwa ukisambaa
kutokea juu ya msikiti huo.
Walisema baada ya
kuona hivyo waliamua kuwajulisha kikosi cha zimamoto kwa kutumia simu zao na
baada ya muda mfupi walifika na kuanza kuzima Moto huo uliokuwa ukisambaa kwa
kasi kuanzia juu ya Olofa ya msikiti huo.
Mmoja waumini hao
alietambulika kwa jina moja la Said alisema waliona moto huo ukianzia juu kwenye maungio ya Umeme sehehemu ya men
swichi ambapo uliendelea kusambaa kabla ya kudhibitiwa na kikosi cha zimamoto
Kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Dodoma
Damas Nyanda aliyefika na kujionea hali halisi alisema walikuwa bado hawajapata
taarifa kama kulikuwa na mtu yeyete aliyejeruhiwa ama kupoteza maisha.
Alisema mpaka wakiti huo walikuwa wanaendele na zoezi la
uokoaji na baada ya mambo yate kuhakikiwa taarifa rasmi ya hasa iliyopatikana
baada ya tahimini ya viongozi wa msikiti huo.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto mkoa Sajenti
Amiry Issa alisema walifika Dakika 4 baada ya kupokea Taarifa ya ajali hiyo ya
Moto na kukuta moto umesamba maeneo mbalimbali ya msikiti huo wenye Olofa moja.
Issa alisema urahisi wa kuzima moto huo ulitokana na wao
kupewa taarifa mapema kabla ya moto kusambaa sana na kuwa na madhara makubwa.
Akatumia Fursa hiyo kuwataka watu kutofanya juhudi za
kuzima mioto yoyote inayojitokeza wenyewe kabla ya kuwajulisha zimamoto maana
kwa kufanya hivyo kunachelewesha uzimaji na kusababisha hasara kubwa
Gazeti hili lilishuhudia Mazuria yanayotumiwa kuswali,
vitabu, kanzu na nafaka iliyokuwa Gorofa ya juu kuwa imeunguzwa na moto huo
uliozuka kuanzia majira ya saa 8. 10 mchana.








No comments:
Post a Comment