Dar es Salaam. Mtoto Kudra aliyekuwa ameunganika na kiwiliwili cha pacha mwenza, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mtoto huyo alifanyiwa upasuaji Alhamisi iliyopita
katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na kulazwa katika wodi ya
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), lakini mwishoni mwa wiki
iliyopita alitolewa katika wodi hiyo.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Pili Hija, alisema hivi
sasa Kudra ananyonya vizuri na kwamba amekuwa akitaka kufanya hivyo kila
wakati .
“Kwa kweli kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zimemweka
hai mpaka leo hii, nilikuwa nimeshakata tamaa kuwa nampoteza mwanangu,
nazidi kumuomba Mungu amwekee mkono wake apone kabisa,” alisema Hija.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika
Hospitali ya Muhimbili, Dk Zaitun Bokhary, alisema mtoto huyo anaendelea
vizuri na mwishoni mwa mwezi huu atafanyiwa upasuaji mwingine.
“Tunamwacha achangamke kwanza, mwishoni mwa mwezi
huu tutamfanyia upasuaji mwingine wa kumwekea njia ya muda ya kutolewa
haja kubwa, kwa kumpasua ubavuni baada ya hapo ataruhusiwa kwenda
nyumbani,” alisema Dk Bokhary.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Kudra alipewa jina hilo Alhamisi usiku, saa kadhaa
baada ya upasuaji kufanyika chini ya jopo la madaktari saba,
walioongozwa na Dk Hamis Shaaban, mtaalamu wa Ubongo na Uti wa Mgongo
kutoka Moi.
Alizaliwa Agosti 18, baada ya mwanamke huyo
kujifungulia nyumbani watoto pacha, huku mmoja akiwa hajakamilika viungo
vyote. Pia, kiwiliwili kilichoungana hakikuwa na kichwa, macho, maini,
figo ila alikuwa na mshipa mmoja wa fahamu ambao ulikuwa umeshikana na
mwenzake na kulazimisha madaktari hao kumfanyia upasuaji.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment