Baba Levo na Diamond wako katika kampuni moja ya Leka Dutigite, na pia ni wasanii wanaowakilisha mkoa mmoja wa Kigoma, lakini pamoja na hayo Baba Levo jana (September 4) kupitia ukurasa wake wa facebook aliwasilisha malalamiko yake kwa mashabiki:
Msikilize hapa
“ZAMANI nilikuwa nikiskia mtu analalamika kaibiwa wimbo au kaibiwa
njia. Nilikuwa naona ni kama maigizo na mtu kutafuta kick ya kupandia
.ila leo nasema wazi DAIMOND PLATNUM amechukua korasi ya wimbo wangu
niliopanga kufanyanae unaitwa SWEATY SWEATY na kuiimba kwenye wimbo wake
mpya NO 1 .. kanizungusha sana kumbe alikuwa na lengo lake…ila baridaa
maisha yanasonga…”
Sikiliza demo ya Baba Levo
Mtandao huu ulimtafuta Baba Levo kutaka kujua
undani wa swala hili sababu imekuwa ghafla tofauti na Dayna ambaye
alianza kulalamika kwenye mitandao hata kabla ya video ya Diamond
kuzinduliwa wala kutoka. Baba Levo anadai kuwa Platnumz ametumia kionjo
kilichokuwa katika kiitikio cha wimbo wake aliotaka kumshirikisha.
Baba
Levo amesema kuwa zaidi ya miezi sita iliyopita alimtafuta Diamond ili
amshirikishe kwenye wimbo wake unaoitwa Sweety Sweety,
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“ Diamond nikamwambia bana nina wimbo wangu hivi na hivi nataka kufanya na wewe akaniambia hamna shida wewe fanya ya kwako halafu mi niachie nini nafasi yangu and then tutakuja tufanye nini tufanye kwasababu wote ni ndugu Leka dutigite na vitu ka izo”.
“Nilipomaliza
kuandika nikamwambia mi bana nimeshamaliza kuandika na kila kitu,
akaniambia niimbie nikamwimbiaaa, akaniambia itabidi uniletee demo kwani
umefanyia wapi huo wimbo, nikamwambia mimi nimefanyia kwa nani kwa mo
fire, au sio bana, akaniuliza Mo fire ndo nani nikamwambia producer
wangu alietengeneza Yalayala, akasema aah kati ya vitu vinavyokufelisha
baba Levo ni kufanya kwenye production ndogo na vitu ka izo nini na
nini, inabidi utafute production ambayo ni kubwa kidogo”.
Baba Levo akaendelea kusema kuwa aliufata ushauri aliopewa na Platnumz na kuamua kuihamishia kazi hiyo kwenye studio nyingine.
Baba
Levo amesema kuwa alianza kupata taarifa juu ya wimbo wa Diamond kutoka
kwa mshikaji wake aliyedai kausikia wimbo wa My Number 1 kwa wanafunzi
wa IFM kabla video haijatoka ndipo akamuuliza mbona ametumia kionjo cha
wimbo wake anaotegemea kutoa..
“kilichokuja kufanyika,
kanizungusha zungushaa badae nikaja nikaambiwa kuna mtu akaniambia ebana
eh Levo eeh, sababu mimi unajua mimi mtu wa maskani nikikaa na wana
nini naimba ili niskie maoni yao, unajua kawaida ya Diamond huwa
anavujisha kwanza nyimbo zake anavujisha ikishavuja then anaskia watu
wanasemaje, akanimabia kuna wimbo mmoja nimeskia IFM wa diamond ameimba
vile vile kama chorus ile ile ya kwako. Nikamwambia ah mimi mbona
sijaskia wimbo nikafatiliaaa nikashindwa kuupata huo wimbo”
Levo
kaendelea kusema watu waliendelea kumpigia simu akiwemo H Mbizo ambaye
pia alimwambia kitu hicho hicho kuwa ameusikia pia wimbo wa Diamond
wenye kionjo cha wimbo wake, lakini Levo alijitahidi kujizuia kusema
chochote mpaka atakapokuja kuusikia wimbo wa Diamond na pia asingeweza
kulalamika kwa wimbo ambao hata mhusika hajautoa rasmi.
Baba Levo
anadai hata wakati Diamond anazindua video yake wiki iliyopita yeye
alikuwa hajabahatika kuusikia licha ya kusikia Dayna akilalamika kuibiwa
beat ya wimbo huo huo mpaka jana asubuhi ndio amefanikiwa kuiona video
hiyo na kuthibitisha kile alichokuwa akiambiwa na watu.
Muda
mfupi uliopita Baba Levo amesisitiza kupita ukurasa wake wa facebook
kuwa Diamond amecopy chorus ya wimbo wake na hatafuti ‘kick’
“NARUDIA
tena nina asilimia 100 DAIMOND PLATNUM amecopy KORAS yangu coz nimekuwa
nikimuimbia kila tunapokutana kwa lengo la kumshirikisha kwenye wimbo
wangu (SWEATY SWEATY) ni zaidi ya miezi saba au nane imepita
akinizungusha tu. na kwa kudhibitisha Hilo mimi nina DEMO 5 za KORASI
yangu ambazo nimefanya kwenye studio mbali mbali Ya kwanza 1 kwa MORE
FIRE magomeni 2 STUDIO SINZA 3 kwa TUDY THOMAS mbezi 4 kwa G BAKUZA
KIGOMA 5 kwa MR T TOUCH mwenge… “Ninaweza kuwasikilizisha watu demo zote
Tano lakini sio kuuachia huo wimbo coz ntaonekana walewale wategemea
KICK. wakati MIMI KWA SASA sihitaji kick ya mtu coz msimu huu nina nguvu
ya kutosha. na nina jiamini.. ukitaka kuamini angalia kilichotokea
FIESTA MTWARA JUZI..”
BONGO 5
BONGO 5



No comments:
Post a Comment