Na mwandishi wetu, Dodoma
WANACHAMA wapenzi na mashabiki
wa timu kongwe ya mpira wa miguu nchini Yanga Afrika tawi la Dodoma
waliopo ndani na nje ya mkoa wa Dodoma wametakiwa kufika kwenye mkutano wa kujadili
masuala ya uzinduzi wa tawi hilo.
Wito huo umetolewa na katibu
msaidizi wa tawi hilo
mkoani Dodoma John Banda, ambapo aliwataka wanachama hao kuhudhuria mkutano huo
kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa tawi utakaofanyika mapema mwaka huu.
Katibu huyo msaidizi aliweka
wazi kwamba pamoja na mambo mengine watajadili namna ya ufunguzi wa ofisi ya
tawi hilo iliyopo mapinduzi klabu barabara ya
Bahi (Bahi Road)
Dodoma ambayo
iko tayari kwa ajili ya matumizi.
Banda alisema mkutano huo
utafanyika jumapili tarehe 15/9/2013
kuanzia saa nne asubuhi katika ukumbi wa mapinduzi klabu na kuwataka watu wote
kuzingatia muda kwani kwa kuanza mapema ni sababu ya kumaliza mapema ili kwenda
kwenye shughuli mbalimbali ikiwepo ufuatiliaji wa ligi za Ulaya zinazoendelea.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Aliongeza kuwa Dodoma ni katikati ya nchi hivyo kuwataka
wanachama mashabiki pamoja na wapenzi wa timu hiyo kufika bila kukosa katika
mkutano huo ili kupanga mambo ambayo yanaweza kuwa mfano wa kuigwa na matawi
mengine kote nchini.
Alitaabaisha kuwa wanatarajia
kuwa viongozi wakuu wa kitaifa wa klabu hiyo kufika mjini Dodoma
na kulizindua tawi hilo
mapema baada ya mipango ya maandalizi ya shughuli hiyo kukamilika
“Tunatarajia kuwaonesha
wanachama wapenzi na mashabiki wa Yanga Tawi la Dodoma ofisi yao ili
kuwarahishia kujua maendeleo ya klabu yao kwa ujumla ili tuweze kupanga kwa
pamoja tofauti na kuzungumzia mitaani mawazo mazuri yaliyopo kwa mashabiki wa
timu bila kufanyiwa kazi”, alisema Banda.




No comments:
Post a Comment