HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TIZAMA HAPA PICHA ZA MWANAMKE ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JNIA, JIJINI DAR ES SALAAM

Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa huyo ambapo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wakati kete hizo zimepelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi. 
 
 ANTHONIA OJO AKIWASILI KITUO CHA POLISI CHA JNIA BAADA KUKAMATWA.
 
 ANTHONIA OJO AKIELEKEA KWENYE GARI BAADA YA KUKAMATWA
  
 AKIZITOA KWENYE MIKEBE YA POWDER NA SHAMPO.ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
 
 PASPORT YAKE
HILO NDO BEGI MADAWA HAYO YALIKUWEMO
 
 AKIZITOA KWENYE MIKEBE YA POWDER NA SHAMPOO
 
SEHEMU YA KETE 99 ALIZOKAMATWA NAZO
HUYO NDO ANTHONIA OJO AKIWA KITUO CHA POLISI
 
MADAWA HAYO YAKIRUDISHWA KWENYE VYOMBO BAADA YA KUONESHWA KWA WANAHABARI.
RECORD ZA ANTHONIA ALIWAHI KUJA TENA MWAKA 2011
Anthonia Ojo (25) Raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya baada ya kukamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana, akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways. Msichana huyo aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwa ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye atafikisha mahakamani. 
Chanzo: Robert Okanda

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: