Umoja
wa Mataifa umesema kuwa takriban wakimbizi elfu 25 kutoka Burundi
wameondoshwa Tanzania kwa nguvu katika mwezi mmoja uliopita.
Afisa
wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi amesema malori
yanayowasafirisha warundi yamekuwa yakivuka mpaka kila siku , huku
wakimbizi wengi wakikosa maji na chakula
Katika
wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwafukuza wakimbizi kutoka
Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo .
Kwa miaka mingi Tanzania iliwahifadhi mamilioni ya wakimbizi waliokuwa wakiyakimbia mapigano katika nchi jirani .
Takriban
watu milioni moja walitoroka kutoka Burundi na kuingia Tanzania wakati
wa mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe wakati vita vilipozuka mwaka 1993.
Wengi walirejea kwa hiari wakati amani ilipopatikana mwaka 2006.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Lakini inaonekana Tanzania haina tena uvumilivu kwa swala hilo. Nchi hiyo imekuwa makao kwa mamilioni ya wakimbizi katika kipindi ya zaidi ya miaka kumi iliyopita kutokana na migogoro katika eneo la maziwa makuu.
Maafisa sasa wameanza kupiga jeki juhudi za kuwaondoa wakimbizi hao kutoka Burundi, Rwanda, na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa nguvu wakiwataka kurejea makwao.
Tanzania inasema kuwa wakimbizi hao ni wahamiaji haramu.
Shughuli hii imetokea wakati mmoja na mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda ambayo imekuwa ikikanusha madai ya kuchochea vurugu katika Jumuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mgogoro ndani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo nao unaendelea kuchochea idadi ya wakimbizi wanaotoroka vita na kuingia katika nchi jirani.
BBC SWAHILI





No comments:
Post a Comment