Askofu wa Dayosisi ya Kati [DCT] Godfrey
Muhogolo akisisitiza jambo kwa waumini wakanisa la Adrea Mtakatifu
Anglikan lililopo veyula manispaa ya Dodoma wakati alipokuwa akizindua
kanisa hilo baada ya ujenzi kukamilika.
Mwenyekiti wa Bakwata wilaya ya chamwino Shekh akisisitiza
jambo kwa waumini wa madhehebu ya kianglikan alipokuwa amekaribishwa
kujionea uwekaji wakfu wa kanisa hilo lililopo Veyula katika manispaa ya
Dodoma.[PICHA NA JOHN BANDA]
Kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ikiwa mbele ya Askofu Godfrey
Muhogolo aliyewaita kuwatambulisha na kuwapongeza kutokana na kusimamia
fedha vizuri zilizotumika kwa ujenzi.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Baadhi ya wachungaji
wakanisa la Anglikan Dayosisi ya Kati wakipewa maelekezo ya namna ya
kuwalisha waumini wa kanisa hilo waliohudhuria uzinduzi jinsi ya
kuwashirikisha meza ya Bwana maarufu kama mkate.
Waumini
wa kanisa la Andrea Mtakatifu Anglikan wakiwa ndani ya kanisa
lililozinduliwa na Askofu wa Dayosisi ya kati Godfrey Mdimi Muhogolo
ujenzi wa jengo hilo ulighalim zaidi ya 194. mil[PICHA NA JOHN BANDA]
Na John Banda, Dodoma
VIONGOZI Madhehebu ya Dini wanaendelea kukerwa na vituko
mbalimbali vikiwemo mipasho na hata kutishia kupigana ambavyo vimekuwa
vikionyesha na baadhi ya Wabunge katika vipindi vya Bunge mjini Dodoma.
Viongozi hao walionyesha hisia za kero hizo mbele ya
waumini wa kanisa la Andrea Mtakatifu Anglikani Paleshi ya Veyula walipokuwa wamehudhuria
uzinduzi wa jingo la kuabudia lililopo kati kijiji hicho kata ya makutupola
manispaa ya Dodoma.
Askofu wa Anglikan Dayosisi ya kati [DCT] Godfrey Mdimi
Muhogolo alisema wabunge wamechaguliwa na wananchi kutokana na kuaminiwa sasa
inashangaza kuona kuwa badala ya kufanya uwakilishi waliotumwa wanageuka kuwa
wapashanaji, kutukanana na kutishiana.
Muhogolo alisema wananchi wanakuwa na matumaini ya
changamoto na yote wanayowatuma wabunge yafikishwe bungeni ili ikiwezekana
serekali iyafanyie kazi badala yake inakuwa kinyume bunge linageuzwa kuwa
majukwaa ya siasa na ulingo wa masumbwi ambayo kabla ya wahusika kupigana huanza
kwa kutambiana.
Aliongeza kuwa wabunge waliochaguliwa na wananchi ni
wasomi kuliko mabunge yaliyotangulia hivyo kama wao wakianzisha fujo bungeni
wananchi wao itakuwaje majimboni mwao na cha kusikitisha zaidi wengi wao ni
vijana wenye nguvu wanaotegemewa sana na Taifa hili.
“Mimi kama askofu naona hayo yote yanatokana na ukosefu
wa hekima, Busara na maadili na ni ngumu kuendesha nchi kwa kutumia nguvu
badala ya hoja, usomi wote ni bure hasa kwa vijana heshima ya mtu haipotezwi na
Siasa kila mtu afanye wajibu wake ipasavyo ili kurudisha imani ya watanzani
kwenye Bunge lake’’, alisema Muhogolo
Nae Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Chamwino Shekh Said
Abubakar Gantana mualikwa katika uzinduzi huo wa kanisa alisema Vitendo hivyo
vya kubishana na kutukanana ni vya aibu kwa watanzania na pia kuaibisha
viaongozi wao wa Dini kutokana na wabunge wote kushiriki kwenye madhehebu
mbalimbali.
Aliwataka wabunge na uongozi mzima wa Bunge kuiga mfano
wa viongozi wa Dini ambao wamekuwa wakishirikiana katika mambo mbalimbali
katika jamii ili kuendelea kuijenga amani na kuimalisha umoja wa kitaifa
uliojengwa na waasisi wa nchi hii waliotangulia akiwemo Hayati Nyerere.
Jengo hilo la kanisa, nyumba ya utumishi,Vyoo Pamoja na
samani vimigharim zaidi ya 194 MIL walizolipwa ili kupisha mradi wa Barabara ya
Dodoma Arusha unaoendelea kwa kiwango cha lami.
Katibu wa kamati ya ujenzi Marry Nghambala alisema walitumia
173,537,950 kujengea na kununua samani za kanisa, ujenzi wa nyumba ya utumishi
ambayo haijakamilika ilitumia 14,466,100 na ujenzi wa vyoo na nyumba za uani
kwenye nyumba ya utmishi 6,730,100 na jumla yake ikiwa 194, 734, 150.
No comments:
Post a Comment