Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza na wakazi wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,filiofanyika leo asubuhi ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU),kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.Kampuni ya Serengiti ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2013 linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja Sokoine.
Muwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea
Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza jambo na msanii wa muziki wa kizazi kipya aitway Niki wa Pili ndani ya semina ya Fursa kwa vijana.
Muwakilishi kutoka shirika la TPSF,Bwa.Louis Accaro akifunguka kuhusiana na mambo ya fursa kwa vijana na nanmna ya kuzichangamkia mara zipatikanapo.
Mdau wa Kilimo kutoka mkoani Mbeya,Bwa.Yona Daniel akizungumzia fursa zinazopatikana kwenye kilimo,ambapo amewaasa vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye suala zima la kilimo.
Semina
ya Fursa kwa vijana ikiendelea.Semina kama hii imekweíshafanyika kwenye
mikoa ya Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara na leo mkoani Mbeya.















No comments:
Post a Comment