Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa
Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar
es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa idara
hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. Dk
Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu. Mkutano huo
ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa
Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar
es Salaam. Dk Nchimbi alifanya ziara ya siku moja katika Ofisi
za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kuzungumza
na watumishi hao masuala mbalimbali ya utendaji kazi
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
- Kamishna wa Pasipoti na Uraia, wa Idara
ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kulia) kuhusu
masuala mbalimbali ya maendeleo ya idara hiyo. Watumishi mbalimbali waliuliza
maswali pamoja na kutoa maoni yao katika mkutano huo uliofanyika katika
Ofisi za Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Kulia
ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto (Meza Kuu) ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja
na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile
Mwakinyule. (Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).



No comments:
Post a Comment