Mwanadada
Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya
watazamaji waliojitokeza usiku wa leo kwenye tamasha la Serengeti fiesta
2013.
Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku wa leo
Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara,ambapo tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku wa leo.
Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva, Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku wa leo, mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva, Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku wa leo, mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku wa leo ndani ya uwanja wa Karume.
Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.
Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku wa leo ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma usiku wa leo
Anaitwa Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta usiku wa leo.

Makamuzi yakiendelea jukwaani usiku wa leo.
Sehemu ya umati wa watu.
Msanii wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga hizo,Neylee akiimba jukwaani usiku wa leo wakati wa tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.
Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa usiku wa leo kwa staili yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume usiku wa leo
Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume usiku wa leo .
Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza.
Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop, Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.
PICHA NA JIACHIE BLOG

No comments:
Post a Comment