HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » YALIYOJIRI KWENYE TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 NDANI YA IRINGA



Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku wa jana kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013
 Mmoja wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake usiku wa leo kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta  linafanyika usiku huu.
Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea usiku wa leo ndani ya uwanja wa Samora.

 ENDELEA KUTIZAMATUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Msanii aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS, Walter Chilambo akiimba jukwaani usiku wa leo, wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora. 
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani usiku wa leo
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa leo ndani ya uwanja wa Samora.
  Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku wa leo mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Ni noma saana
Anaitwa Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe za mashabiki zikivuma kila kona ya uwanja.
 Anajiita Rais wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wa Nani kaiba yangu usiku wa leo kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,linalofanyika ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mmoja wa madansa machachari sana kutoka THT,aitwaye Msami akiwa amebebwa juu na mashabiki baada ya kuonesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma jukwaani.
Wasanii wanaokuja juu katika anga ya muziki wa kizazi kipya-hip hop.Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku mayowe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja.

 

  Pichani ni sehemu ya wakazi wa Mkoa Iringa na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku wa leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linaloendelea kufanyika hivi sasa katika uwanja wa Samora.
HABARI NA JIACHIE BLOG 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: