JESHI la Polisi limewafukuza kazi askari wawili wa Kituo cha Polisi cha
Mugumu mkoani Mara, baada ya kukamatwa na jino moja la tembo lenye uzito
wa kilo 3.5. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ferdinand Mtui, aliwataja
askari hao kuwa ni D/CPL Isack (43) mwenye namba E.9069 na D/C Sixbert
Amos (25) mwenye namba F.5580 kwa kushirikiana na John Sogita maarufu
Masese ambaye ni mkazi wa eneo la Bomani mjini Mugumu, walipatikana na
nyara hiyo katika eneo la Kisima cha Mafuta cha EAFCO kilichopo wilayani
Serengeti.
Alisema askari hao walikamatwa Oktoba 25, mwaka huu, saa nne usiku
na askari wa wanyamapori wakitumia Toyota Caldina lenye namba za usajili
T 269 BRN mali ya askari Amos.
Alisema kukamatwa kwa jino hilo
kumetokana na operesheni okoa maliasili, iliyoendeshwa na askari hao na
chanzo cha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni harakati za kutafuta mteja wa
kulinunua.
Alisema askari hao wameshitakiwa kijeshi na
wamefukuzwa kazi Novemba 7, mwaka huu na wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani wakati wowote.
RAI




No comments:
Post a Comment