Mwigizaji na mchekeshaji maarufu, King Majuto amesema anaogopa kualikwa katika matamasha ya nje ya nchi kwasababu anaweza kukwama kama Kingwendu alivyokwama Kongo.
Akizungumza na mtandao huu leo, Majuto alisema alitembelewa na watu wakimtaka akafanye maonyesho Burundi ila ameshindwa kukubaliana kwasababu ya kuogopa kukwama kama ilivyotokea kwa Kingwendu aliyekaa miezi sita, DRC.
“Hapa kwangu jana walikuja watu wa Burundi wakihitaji nikafanye show,ila sijaelewana nao kwasabu hawajajipanga vizuri. Isije ikawa kama ya Kingwendu alikwenda Kongo akakaa miezi sita bila kurudi nyumbani,” Majuto aliuambia mtandao huu
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Kingwendu alinipigia simu akaniambia yupo Kongo, hana pesa ya kurudia Dar es Salaam anahitaji msaada. Watu waliompeleka wamemtapeli Hana cha kufanya,akaniambia nipeleke angalau unga kwa watoto wake kwasababu hajaonana nao kwa miezi sita.”
BONGO 5




No comments:
Post a Comment