Bob Junior, mke wake na mtoto wao
Magazeti ya udaku yameendelea kumwandama Bob Junior kiasi ambacho ameamua kusema ‘inatosha sasa’
Kupitia
mitandao mbalimbali ya kijamii anayoitumia staa huyo, Bob Junior
ameyalaani magazeti hayo kwa kuendelea kuikuza habari ya kuachana na
mkewe wake kutokana na kile yalichodai kuwa (mkewe) alikuta nguo ya
ndani ya mwanamke mwingine.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“Ahsanteni sanaa hii imekuwa too much sasa kila nikiomba muache hamtaki hamna story nyenginee jamanii,”ameandika Bob Junior kwenye picha ya gazeti la udaku lililoandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho: Kufuli ya kike aliyofumaniwa nayo Bob Junior ni yake’.
Juzi pia alilalamika baada ya gazeti la udaku kuandika habari yenye kichwa cha habari: Ndoa ya Bob Junior Chali.
“Leo tena jamani hakuna habari nyingine hata kama nimeachana naye kanizalia napaswa kuwekewa heshima mwanangu akija kuwa mkubwaa nita mwambia nini mimi inaniumaa Bob Junior tuu akilala akiamkaa ni Bob junior kila sehemu.”
Habari ya kwanza kuandikwa na gazeti hilo la Sani kuhusiana na kisa hicho ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho: Sidiria, Chup* yavunja ndoa ya Bob Junior.”





No comments:
Post a Comment