Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake
chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakiwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji
katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako
Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1.
Nahodha wa The Tanzanite, Fatuma Issa akizungumza na waandishi wa habari.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura akipeana
mkono na wachezaji wa Tanzanite mara baada ya timu hiyo kuwasili jijini Dar es
Salaam ikitokea Msumbiji.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wachezaji
The Tanzanite wakiwapungia mikono mashabi waliofika kuwapokea kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, wakitokea
Msumbiji.
Hapa ilikuwa ni furaha baada ya ndugu kukutana
Kocha Mkuu wa The Tanzanite, Rogasin Kaijage akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuwasili nchini
Mchezaji wa The Tanzanite, Anastazia Anthony akiwa na kaka yake Nickodem Anthony baada ya kuwasili nchini wakitokwa Msumbiji
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura akizungumza na vyombo vya habari baada ya timu ya Tanzanite kuwasili jijini Dar es Salaam ikitokea Msumbiji.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao baada ya kuwasili jijini Dar es Salam wakitokea Msumbiji.
Wachezaji wa timu ya taifa ya wananwake chini ya
umri wa miaka 20 'Tanzanite' wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea
Msumbiji katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia la wanawake dhidi ya
Msumbiji, ambako Tanzania ilishinda 5-1.
Baadhi ya wachezaji wa timu
ya taifa ya wanawake
chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakipanda basi baada ya
kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji.







No comments:
Post a Comment