Vinara wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wamekutana na kipigo kikali kutoka kwa Manchester City cha mabao 6-3 katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester. Kutokana na kipigo hicho Man City imefikisha pointi 32 wakati Arsenal imebaki kileleni ikiwa na pointi 35.
Mabao ya Man City yamefungwa na Sergio Agüero katika dakika ya 14, Álvaro Negredo (39), Fernandinho (50 na 88) na David Silva (66).Theo Walcott aliifungia Arsenal mabao mawili katika dakika ya 31 na 63 kisha Per Mertesacker akaongeza la tatu katika dakika ya 90.
No comments:
Post a Comment