HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » FAINALI YA TPF6 YAHARIBIWA NA VIDEO ‘MBOFUMBOFU’ ZA WASHIRIKI WALIONGIA TOP 5


Fainali za shindano la Tusker Project Fame msimu wa 6 zilianza kwa kishindo kwa matumbuizo yaliyowavutia wengi. Kwenye fainali hizo pia, washiriki wote na walimu wao walijiunga pamoja kuimba wimbo wa heshima kwaajili ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyefariki wiki hii.

Baada ya hapo washiriki waliokuwa wameingia top 5 walipanda pamoja na washiriki wengine wa zamani wa shindano hilo na kuimba nyimbo mbalimbali za zamani, burudani ambayo ilipendeza sana.
Sura mpya zilizorudi tena kupanda jukwaa hilo la TPF, ni pamoja Msechu, Patricia, Davis wa Uganda, Wendy na mshindi wa mwaka jana, Ruth Matete wa Kenya.
Baada ya hapo washiriki hao watano wakaanza kupanda mmoja mmoja kuimba nyimbo walizozirekodi wenyewe. Hisia wa Tanzania alianza kwa kuimba wimbo mzuri wenye mahadhi ya house za Afrika Kusini na uliotengenezwa na producer nguli wa Kenya, Erick Musyoka.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Wimbo huo ulikuja kutiwa doa na video yake iliyooneshwa kipande. Video hiyo inayoonekana wazi kuwa ni bei cheee, iliharibu uzuri wote wa wimbo wa Hisia. Ni video mbaya, yenye kiwango cha chini sana na ambayo kwa hakika iliwaacha mdomo wazi watazamaji wengi hasa wakizingatia kuwa waandaji wa shindano hilo si watu wa kubabaisha. Ilikuwa ni video mbaya ambayo mtu aliyeitengeza huenda alikuwa ameanza kujifunza fani hiyo.
Baadaye Hope naye alitumbuiza wimbo na video yake ilipoweka, mambo yalikuwa yale yale. Hata video za Daisy na Amos na Josh zote zilikuwa na kiwango cha chini vile vile. Video hizo zikachafua hewa na kuifanya hashtag ya #TPF6 kwenye Twitter kulipuka na madongo yaliyozikosoa video hizo zilizo chini ya kiwango.

Hizi ni baadhi ya tweets hizo:

jimmy nyoike: Those videos can make a pig puke!! tusker what is happening to your quality control!? some songs r good tho but vids RIVER ROAD!!

patrick muchiri: Awesome show… But hizo video! Hapana! Haziwezi!!!
Ciiru Kang’ong’oi: Whoever idea IT. Was with this #TPF6. Music videos.. Ichieny
Deehlovely: Eish, the videos done for the new singles on #tpf6 are just super low. I hope they plan on making new videos
Modesta: The videos be killing the songs jamaneni
Deejay Sylar: Is it me ama its true ths #TPF6 Videos are #whack?? Ain thy just wasting tha nicely written and produced songs??
Social Experiment: Good god, was Daisy’s video shot on a Nokia???? It looks bad, bad – at Luche will never make such a video #tpf6
˚MaRy MuThOnI˚: I wish they didn’t do those videos!!audio would be enough for me aaaaiiii kuwa shady nayo #tpf6
Crazy Kenyan: The quality of the videos on #TPF6 are the reason why most Kenyan music never hit worldwide
David Mugo: #tpf6 should not have rushed to do videos. The music is great but the videos are crap
Kevo Kish: One thing that these contestants will learn from the outside world is that such music videos just can’t hack it
Kwa kukoselewa huko, bila shaka uongozi wa Tusker Project Fame utafikiria kushoot upya video hizo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: