HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » LULU ADAI KUKOSESHWA AMANI NA SIMU YAKE,SIIHITAJI KWA SASA


Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu, amesema kuwa hatamani tena kutumia simu ya mkononi kwakuwa anasumbuliwa mno na watu wasiokuwa na mambo ya msingi huku akitamani irudi enzi ya kutumiana barua.

Akiongea na gazeti la Mwananchi jana,Lulu alisema kuwa kero hiyo humfanya atamani kurudi katika enzi za kale za kuwasilia kwa kutumiana barua kwa njia ya posta.
“Nadhani sihitaji simu ya mkononi kwa sasa, mwenye shida na mimi atanitumia barua. Sijui, hata sijielewi nikasimame wapi, maana hata nikibadili nambari ya simu inasambaa kwa kasi sana,”alisema.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Lulu alibainisha kuwa kwa siku hupigiwa simu zisizokuwa na idadi na zisizo na faida kwake, lakini akakiri kwamba idadi kubwa ya watu wanaompigia simu ni mashabiki wake.
“Ninapigiwa simu nyingi kwa siku ambazo ni kero kwangu, nafurahi sana ninapopigiwa simu na shabiki wangu, lakini wapo wanaopiga simu kutaka mambo ya ajabu. Sawa ni wengi wao ni mashabiki wangu, lakini simu kwangu ni kero kubwa ingawa ni msaada mkubwa pia kwangu ni sehemu ya kitendea kazi.”

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: