Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela Jumapili hii amezikwa kijijini kwake alikozaliwa, Qunu katika jimbo la Eastern Cape nchini Afika Kusini katika mazishi yaliyohudhuriwa na watu takriban
5,000.
Kwaheri Madiba: Jeneza lilibeba mwili wa Mandela likiingizwa kwenye kaburi lake lililpojengwa jirani na makaburi ya wazazi wake
Jeneza lake lilikuwa limebebwa kwenye gari la kubebea silaha na kupelekwa kwenye makaburi ya familia. Wakati mwili wake ukiwekwa kaburini, bendera ya Afrika Kusini iliondolewa na kukabidhiwa kwa mjane Graca Machel, aliyekuwa akiliwazwa na mke wa zamani wa Mandela, Winnie Mandela.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Jeneza la Mandela likiwa limezungukwa na maafisa wa juu wa jeshi
Hata hivyo ratiba ya mazishi hayo ilizidisha muda kwa karibu masaa mawili na hivyo mila za kikabila kuwa mazishi yanatakiwa mchana wakati jua likiwa utosini ilibadilika.
Mandela alifariki December 5 akiwa na umri wa miaka 95.
Helikopta za kijeshi zilizokuwa zimebeba bendera za Afrika Kusini zilipita juu ya kaburi ikifuatiwa na saluti ya risasi 21
Wageni waliohudhuria ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete na marais wengine wa Afrika, Prince Charles, Oprah Winfrey, Richard Branson mwanaharakati wa Marekani, Jesse Jackson.
Oprah Winfrey (katikati) akiwa na mume wake Stedman Graham (kushoto) na bilionea wa Uingereza Richard Branson
Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma akzungumza wakati wa mazishi ya Mzee Nelson Mandela
Ilikuwa ni simanzi
Mjukuu wa Mandela, Nand akiongea mbele ya waombolezaji huko Qunu
Mke wa zamani wa Mandela Winnie (kushoto) Rais Jacob Zuma na mjane wa Mandela Graca Machel
Mtoto wa Mandela Zindzi akimliwaza muombelezaji mwingine
Mjane wa mzeee Nelson Mandela, Graca Machel, akiwa na mke wa zamani wa Mandela, Winnie Mandela wakati wa mazishi ya Hayati Nelson Mandela
Mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela akilitizama jeneza la babu ake Hayati Nelson Mandela
Viongozi wa kijeshi wakiweka picha ya bendera ya taifa yaAfrika ya Kusini kwenye jeneza la Hayati Nelson Mandela
Prince Charles akisalimiana na wageni wengine
Wakazi wa Qunu wakishuhudia kwa mbali mazishi
Wengine walitizamia kwenye luninga
Ulinzi ulikuwa ni wakutosha kwenye mazishi ya mzee Nelson Mandela
No comments:
Post a Comment