Wote tunapenda biashara zenye mafanikio, lakini hatujui tufanye
nini. Wengi tunaanzisha biashara ya kuiga tu, ingawa sijasema kuiga ni
dhambi,basi utakuta salon hapa, pale, kule, nyuma, mbele pembeni yam taro
wengine hata mteja akija anashukuru Mungu ndio anaagiza na chips kabisa ili
afukie mashimo ya njaa. Mbaya zaidi
huduma kwa wate sio nzuri kwa kuwa biashara yenyewe haina lengo lolote zaidi
mtu anajua kusuka, hakuna maandishi (Business Plan), lengo la biashara kuwa
baada ya muda Fulani nikuze biashara yangu kwa kuongeza jingo labda nk.
Wengi tuna nunua magari ili yawe Taxi lakini hii Taxi haina
mafanikio hata kidogo kwa kuwa dereva analalamika gari limekuwa si gari na sasa
ni jinni, maana linbugia mafuta balaa, ukija kwa madereva wenyewe sasa hawana
mission wala vision, wao ni kubambika tu bei mteja anapanda taxi mwaka mzima
wewe umeng’ang’ania bei kubwa hadi anakukimbia, lakini kama ukijipanga kwa
lugha, bei nzuri, service ya gari, uaminifu utafanikiwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakati najiingiza katika biashara nilikuwa nafanya kwa moyo
mmoja kwa kutaka kushirikiana na wenzangu hata ikiwezekana tuchange tuweze
kufanya biashara moja ambayo itazalisha na kupata faida kubwa.
Lakini kumbe wenzangu walikuwa na malengo yao, walifanikiwa
kuchukua mitaji kutoka kwangu na nilibaki masikini mwisho niliamua kuhamia
katika biashara nyingine ambayo nilihisi itanizalishia. Nilijiunga lakini bahati mbaya nilisahau kuwa
hiyo biashara nipo na wale wale walioniangusha, na nilianguka kweli kwa kuwa
nilipoteza fedha, nilipoteza marafiki, niligombana na mke wangu, nilikuwa na madeni ambayo hadi leo
ninaendelea kulipa.
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta
na kuendesha aina ya ile biashara unayotaka kuifanya, lakini pia ni vyema
kubuni mradi unaoweza kuendelea, sio ule ambao unaanzisha leo, kesho unakufa
Jambo linguine la msingi ni kujenga tabia ya kuweka akiba.
Lakini la tatu kali zaidi ambalo wengi wetu huwa ni gumu ni
ushirikiano wa watu zaidi ya wawili, ambao mna nia moja katika jambo moja mfano
salon.
Ikiwa salon inahitaji vifaa vya kisasa basi hakikisha wazo lenu
liwe la vifaa vya kisasa, mfano hesabu zenu ziangukie kuwa na viti 100 vya
wateja wanaofanyiwa usafi wa nywele, viti 100 ambavyo kuna wateja, wanafanyiwa
steaming, viti 100, ambavyo kutakuwa na wateja wanaoshwa miguu, viti 100 vya make
ups, madawa yaliyoidhinishwa na TBS na TFDA ambayo hayadhuru mteja, huu ni
mfano tu na pia unawea kuona katika picha nilizoweka.
Mnapokuwa mmeungana nguvu inakuwa ni kubwa kazi yenu ni
kusimamia kila mmoja kujua anafanya kazi kwa umakini, analipwa kama mkataba
unavyosema, usafi wa ofisi, lugha nzuri kwa wateja, ratiba zinaenda kama
zilivyopangwa, wahudumu wanakuwa na muda wa kupumzika na huku wakiwa huru
kwa wenye ofisi katika kusema yao yaliyo moyoni, mfano kutoa
mawazo yao na yakanyiwa kazi, mikutano ya kila wiki mfano jumatatu na ijumaa
huwa inazalisha utendaji kazi uliomakini, lakini mikutano ya kila siku asubuhi
au jioni kwa wenye biashara ni muhimu.
Mnaweza kujiunga watu 10 mabao mtaamua kuchanga labda
5,000,000/= kila mmoja ukipiga hesabu 5,000,000 x 10 = 50,000,000/= mnaweza
kupanga kimkataba kuwa tutafanya kazi kwa umoja kwa miaka mitano baada ya hapo
tutaangalia kama inalipa ili tuendelee, au kila mmoja aende kivyake.
Ili upate mafanikio kwa karne hii ya 21, ni lazima uweke
ushirikiano na wenzako bila hivyo utaimba kama nguchiro, na kila siku utabaki
kukataa na kuona kila jambo ni baya katika biashara yako.
Kitu kingine kikubwa ni kuwa na muda au ratiba maalumu na
inayotekelezeka katika biashara yako, mteja akija anataka baridi katika chumba
iwe baridi sio kila siku wewe unakuwa mama samahani au baba samahani, hawa
Tanesco hawa, hapana ingia mkataba na kampuni la umeme wa jua, au upepo, ili
wateja wako wapate huduma
ile ile au zaidi ya ile na sio kila siku unapunguza ukarimu kisa anakuja kwako
hana pa kwenda, weka vitu kama vinywaji hasa hasa sharubati za kutengeneza
mwenyewe kwa matunda ya msimu na yale yanayopatikana iwe katika hali ya usafi. Au chukua paketi moja ya Tanga Fresh mtindi
na ndizi tano mbivu sana weka katika blender hakikisha una blend kwa sekunde 40
hadi 60, wape bilauri ndogo wateja wako wawili wanywe utaona
kesho watakuja kuuliza kama ulinunua wapi kinywaji kile, maana utakuwa
umewasaidia sana kiafya, na ladha pia.
Hili ni somo nitakupa baadaye.
Biashara sio kila dakika ufikirie kupiga hesabu watakuja wangapi
wateja, biashara ni jinsi gani kwanza hawa ulionao wataendeleaje kuja ili nao
wakuletee wateja wengi, weka motisha au zawadi kwa wateja akikuletea wateja 10
yeye atapata shampoo moja au shilingi 10,000 au hata kufanyiwa huduma bure.
Mafanikio hutokana na jitihada katika maisha tunayoishi. Watu wengi wanaopenda kufanikiwa hutafuta
mbinu mbalimbali za kutimiza ndoto zao.
Je wewe unafanya nini kutimiza ndoto ambazo umekuwa nazo kwa miaka mingi
kwamba nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa.
Waza unipe jibu, tupeane
mawazo.
Imeandaliwa na Buberwa Robert
















No comments:
Post a Comment