Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Chididimo waliojitokeza
kumlaki alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji kijijini hapo jana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi(kushoto) akipokea taarifa ya mradi wa maji kijiji cha
Chididimo manispaa ya Dodoma kama inavyowasilishwa kwake na mhandisi
Mohamed Khali ( Kulia) kutoka idara ya maji manispaa ya Dodoma
wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika jana.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
akizindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma jana, wengine ni wajumbe wa chombo huru cha watumiaji maji kijijini
hapo.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasha
mashine ya kusukuma maji kwenye mradi wa maji kijiji cha Chididimo
manispaa ya dodoma muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
(kushoto) akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa kijiji cha Chididimo kilichopo
manispaa ya Dodoma kuulinda na kuutunza mradi wa maji kijijini hapo muda
mfupi mara baada ya mkuu huyo wa mkoa kuuzindua mradi huo jana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi
(kulia) na katibu tawala Mkoa
Dodoma Ndg. Rehema Madenge wakifungua na kukinga maji kwenye mradi wa
maji kijiji cha Chididimo kilichopo manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi
huo mapema jana. Wanaoshuhudia ni wananchi wa kijiji cha Chididimo.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi
akimtwika
ndoo ya maji mdala Morleni Mwaluko mmoja wa wanakijiji cha chididimo,
maji hayo safi kwa sasa yanapatikana kwa urahisi na kwa karibu
kijijini hapo baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa kijiji hicho,
mkuu wa MKOA dodoma amezindua mradi huo mapema jana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi
(aliyeshika kibuyu katikati) akiimba na kuserebuka nyimbo za asili ya
kigogo pamoja na akinamama wa kijiji cha Chididimo manispaa ya Dodoma
kusherehekea muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua mradi wa
maji kijijini hapo jana.
No comments:
Post a Comment