Moja ya Shimo la magadi soda katika Bonde la
Engaruka.
Picha inayoonesha moja ya mashimo yaliyochorongwa katika Bonde la Engaruka Wilayani
Monduli, Mkoa wa Arusha kuthibitisha uwepo wa hazina kubwa ya magadi soda. Hii
ilidhihirishwa mbele ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango
aliyeongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka katika ofisi yake (hawapo
pichani).
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto) akionja maji ya magadi soda yaliyotoka katika moja ya shimo lilichorongwa katika bonde la Engaruka alipoongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango. Anayewamiminia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bw. Gideon Nasari.
Timu
ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakijaziwa maji ya
magadi soda katika chupa za maji ya kunywa walipotembelea bonde la Engaruka
ambako kuna hazina kubwa ya magadi soda.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt.
Philip Mpango akitazama (admires) kipande cha magadi soda katika eneo la Ziwa
Natron Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha alipoongoza timu ya wakaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoka katika ofisi yake. Pamoja naye ni watoto wa kimasai
waliokuwa wakiuza vipande hivyo vya magadi soda.
No comments:
Post a Comment