HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » UPDATES:SOMA HAPA HABARI KAMILI MGOMO WA DALADALA MOROGORO

MADEREVA wa daladala Manispaa ya Morogoro wamegoma asubuhi hii wakidai 
kukamatwa hovyo na matrafiki na hakuna daladala linalofanya safari yoyote katika manispaa hiyo.


Madereva hao wanadai wameamua kugoma kutokana na kamatakamata ya askari wa  usalama barabarani, ambapo wamesema daladala moja kwa siku linaweza kukamatwa hadi mara nne na wakihoji wanaambiwa ni makosa tofauti.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Waliongeza kuwa wamepeleka malalamiko yao ngazi mbalimbali za serikali mkoani  Morogoro bila mafanikio.


Mgomo huo umewaathiri zaidi wanafunzi ambao wapo katika mitihani ya nusu muhula  ambapo baadhi yao walilazimika kutembea kwa miguu huku wengine wakirudi nyumbani kujipanga.


Ili kuongeza uzito katika mgomo huo, madereva hao wametoa tahadhari kwa wamiliki  wa mabasi ya Abood kutojaribu kupeleka mabasi yao barabarani kama ambavyo wamekuwa wakifanya pindi ukitokea mgomo ndani ya manispaa hiyo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: