Mkuu wa Mkoa wa Dodoma DKT Rehema Nchimbi kitoa maelekezo kwa watendaji hao wakuu wa serikali ngazi za Halmashauri.

Meneja wa Wakala wa Barabara Renald Shimagu akizungumza jambo wakati
alipokuwa akifafanua jambo kuusu ujenzi wa barabara uanaoendele mbele ya
kamati hiyo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wabunge na wenyeviti wa Halmashauri Mkoani
Dodoma wakiwa katika kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) kilichofanyika
juzi na jana na kutoka na maadhimio mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wiliya ya Kondoa Hamis Mwenda akifafanua
jambo wakati alipokuwa akichangia jambo wakati wa kikao cha ushauri cha
mkoa wa Dodoma (RCC)
Meya wa manispaa ya Dodoma Emanuel Mwiliko alitoa mchango wake wa mawazo.
Mbunge wa Viti Maarumu Mariamu Mfaki alikutoa mapendekezo yake katika kikao hicho cha siku mbili.
Na John Banda,Dodoma
WABUNGE wa Mkoa wa Dodoma wameshutushwa na baadhi ya kauli
za Wajumbe wa Bunge la Katiba za kutaka kuwe na kipengele katika Katiba ijayo
cha kuhamishia Makao Makuu ya Serikali kuwa
Dar-es-Salaam badala ya Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa jimbo la Bahi Omar Badwel kwenye
kamati ya ushauri ya Mkoa wa {RCC) alipokuwa
anachangia kuhusu maendeleo ya kuhamia
makao makuu ya serikali kuhamia Dodoma.
Mbunge huyo ambaye
pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba alisema hayo kutokana na baadhi ya
Wajumbe wa kamati za Bunge kutoa mapendekezo yao na kutaka makao makuu ya Serikali kuyataka yahamie Dar-es-Salaam badala ya Dodoma.
Alisema wajumbe hao
wametoa mapendekezo hayo kwa kigezo kuwa toka Rais wa kwanza wa Jamhuri ya
Muuungano Mwalimu Julias Nyerere atamke mwaka 1973 kuwa Dodoma iwe Makao Makuu
jambo hilo halijatekelezwa mpaka sasa kutokana shughuli nyingi na Wizara nyingi
kufanyia Dar-es-Salaam badala ya Dodoma.
Omar alisema kutokana na madai hayo Wajumbe hao wamesema
kuwa serikali inaonekama suala hilo ni
kama kiini macho kwa Watanzania ambao
waliamini kuwa kauri ya Nyerere ingeweza kutekelezwa toka ilipotolewa juu ya
kuhamishia Dodoma kama makao makuu ya serikali.
Mbunge huyo ambaye katika kundi lake kuna wabunge wapatao
wanne wa Dodoma waliopangwa katika kundi lililopo Dodoma Hotel,na wengine
kupangwa kwenye kamati maeneo mengine’
Hata hivyo Wabunge wa Mkoa wa Dodoma wamelipiga suala hilo
kwa nguvu zote na kusema kuwa hata kama wajumbe hao watalipitisha wao watalipeleka kwenye kikao cha Bunge kwa ajili
ya kuipeleka hoja hiyo ili iweze kujadiliwa na wabunge wote.
Kutokana na suala hilo ambalo liliwashitua baadhi ya wajumbe
wa kikao hicho cha ushauri cha mkoa ambacho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema
Nchimbi alikuwa ni Mwenyekiti wake,kwa upande wake alishitushwa na kusema kuwa baadhi ya maeneo ambayo
yalitengwa kwa ajili ya kujenga kuwekezwa na serikali kuuzwa.
Dkt Rehema alisema baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa
yametengwa kwa ajili ya serikali tayari yamezungushiwa fesi suala ambalo
linaloonyesha wazi kuwa uhamiaji wa makao makuu ya serikali utekelezaji wake hauchukuliwi
kwa mkazo kama ilivyoamuliwa na serikali.
‘’Oneni wenyewe eneo la ihumwa kuelekea chamwino ambalo
lilikuwa maarumu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ambapo eneo hilo lingejulikana
kama mji wa kiserikali tayali limeanza kuzungushiwa wigo haliinayoashilia
tayali limeuzwa hapa itabidi Mamraka husika watuambie CDA si mpo’’, alihoji
Nchimbi
Alisema inawezekana hayo ni maoni yao lakini sisi tunaamini
kuwa Dodoma bado ni makao makuu ya serikali mpaka hapo itakavyotolewa kauli nyinginezo
za kuyahamisha.









No comments:
Post a Comment