Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Jeshi
la
Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu nane kwa makosa mbalimbali ya
uhalifu kufuatia msako uliofanyika tarehe 01/04/2014 maeneo mbalimbali
ya Mkoa wa
Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tukio
la kwanza alikamatwa SIMON S/O MTUNDU, miaka 51, Kabila Mhehe, mkulima na mkazi
wa kijiji cha Kisisi Kata ya Kimagiyi Tarafa na Wilaya ya Mpwapwa, akimiliki
silaha aina ya Gobore lenye Namba MP. 00202182 kinyume cha sheria za umiliki wa
silaha.
Kamanda MISIME amesema tukio jingine alikamatwa CHISEMI S/O ROBERT, miaka 34, kabila Mgogo, mkazi wa kijiji
cha Kiboriani Wilaya ya Mpwapwa na wenzake wawili wakimiliki shamba la bhangi
ekari moja na nusu (1.5) kinyume cha sheria. Shamba hilo limefyekwa na kuteketezwa
kwa moto.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Aidha katika Wilaya ya Chemba Mkoani humo alikamatwa MUSSA S/O ALLY MADEBE, mwenye miaka 20, mkulima wa
Kijiji na Kata ya Songolo Tarafa ya Goima na wenzake watatu wakiwa na misokoto
nane ya Bhangi, watuhumiwa watafikishwa
mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na msako bado unaendelea.
Kamanda MISIME amewashukuru wananchi hawa wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa
taarifa na kushirikiana na Polisi katika misako.
No comments:
Post a Comment