By Mark Rose Msemwa
Kwanza nawapa pole wote waliokamatwa na Sikukuu ya wajinga. Pia nipingane na fikra ya kuwa wao ni wajinga kwani kutambua kuwa nilichofanya/nilichoamini ni ujinga basi hiyo ni hatua ya kuondokana. Ni siku nyingine tena ndugu msomaji ambapo tunakutana kwa njia ya maandishi kwenye mwendelezo wa namna ya kumfanya mteja awe teja wa huduma yako tukiwa tunahitimisha makala hii.
12; Kuwa msikivu hata unapokosolewa. Kuambiwa huduma yako mbovu na mteja au mtu mwingine tu, ni jambo la kawaida kabisa katika maisha yetu ya kila siku, madhara yake itategemea na wewe ulieambiwa unapokeaje na unatafsiri gani juu ya hilo. Kumbuka mtu hadi akuambie kuwa huduma yako mbovu ni lazima atakuwa ashaona iliyo bora kuliko ya kwako, so mwombe akueleweshe ili ujirekebishe huku ukionyesha utayari wa kuelekezwa na kujifunza, katika kazi yangu walimu wangu wakubwa wamekuwa ni wateja. Wateja ni walimu wazuri sana ukiwa msikivu kwani wanapita sehemu tofauti na kukuhudumiwa na watu tofauti.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
13; Tambua kuwa mteja ndio bosi wako wa kwanza, hivyo kumheshimu boss kupita kiasi kuliko mteja ni kazi bure, kwani bosi anakulipa sehemu ya faida anayoipata kutokana na huduma yako. Huwa inanishangaza kuona wafanyakazi wengi wanapomheshimu na kumwogopa bosi zaidi ya mteja, mteja wanamjibu wanavyotaka muda mwingine jeuri, akiwepo bosindio wanakuwa na kauli nzuri na heshima kwa wateja. Wake uuuuup my people! Tutasimamiwa hadi lini!? Kumbuka usipojiongoza siku zote utaongozwa, usipojisimamia siku zote utasimamiwa tu. Heshima unayompa bosi iendane na unayompa mteja. Hapo ndipo utakuwa huru maishani mwako.
14; Shauri/Pendekeza. Wateja wengi kama ilivyo kwa watu wengi huwa hawajui wanachotaka, ni jukumu na sehemu ya kazi yako kumshari na kupendekeza ni nini kitamfaa, ukiingia kwenye maduka mengi wahudumu walio wengi wana mfuata mteja nyuma nyuma utadhani wanamlinda ili asiibe!! Jaribu kuwasiliana nae anataka nini kama hajujui pendekeza kitu cha kumfaa. Muhimu; hakikisha ushauri na pendekezo lako ni kwe linamfaa mteja sio ilimradi uingize pese tu.
15; Tabasamu muda mwingi. Kama ilivyo kwa binadamu yeyote kuzaliwa na mwishoe kufa, pia tumeumba na usawa kitu kimoja tu, ambacho ukiwa nacho ‘you look sooooo beautiful, you look soooo handsome, haijalishi uko vipi and that is your SMILE, una uwezo wa kuibadili dunia kwa tabasamu lako tu. Hivyo hata wateja wanahitaji kuona hilo kwako hata pale unapokuwa na wakati mgumu kumbuka hili. Ila tu kama mteja wako unamwona ana huzuni, jaribu kuendana na hali aliyoyonayo japo sikushauri akilia na wewe ulie, ila tu mpe pole. Mf; siku moja kazini kwangu niliweka CD ya Lionel Richie wimbo wa ‘Hello’ ulipoanza mteja wangu akaanza kuufuatisha, ulipofika kati kati akaanza kutoa machozi, ikanibidi niitoe ile CD na kumpa pole. Na kazi ikaendelea, katika hali kama hiyo huwezi kutabasamu.
Kama haya yote yamenifaa mimi, kunitoa kwe kipato cha 3,000 – 1,700,0000 kwa mwezi ndani ya miaka 10 tu, basi naamini yapo yatakayokufaa pia.
NJIA 15 ZA KUMFANYA MTEJA APENDE HUDUMA YAKO
Tag:
No comments:
Post a Comment