Leo Jumatatu, Aprili 7, Redio yako ya Kijamii ya KwanzaJamii
imeandika historia kwa kuwa redio ya kwanza hapa nchini kuwaletea
wasikilizaji dondoo za habari za magazetini kutokea kwenye soko lenyewe
la habari, ni pale kona ya Uhuru na Msimbazi, Kariakoo.
Ni kipindi cha kila siku kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri. Mwandishi/ Mtangazaji
wa KwanzaJamii atakuwa sokoni hapo na kuungana moja kwa moja na studio
za Kwanzajamii radio Iringa.
Sambamba na redio, habari hizo na picha za magazeti yenyewe
zitarushwa pia kwenye Mjengwablog.com. Ikumbukwe, Mjengwablog ilikuwa ni
blogu ya kwanza hapa nchini kuanza kurusha kwenye blogu dondoo za
magazetini.
Usikose kufuatilia na kuzipata habari zikiwa motomoto kutoka Soko la
habari Kariakoo.
bofya hapa hapa chini kusikiliza



No comments:
Post a Comment