Kundi la Muziki wa kizazi kipya lijulikanalo kama "Wadananda" limebahatika kuingia mkataba na Record label mpya nchini Tanzania ya "Brainstormusic". kampuni hiyo inayomsimamia msanii maarufu wa kizazi kipya " CPwaa" imeamua kujitanua na kuanza rasmi kusimamia kazi na wasanii wa muziki,filamu,Michezo, Michoro,Vinyago,Upigaji picha pamoja na fashion.
Wadananda linalotengenezwa na vijana wawili "Kea Ahmedi kidato"(Customer Care) na "Natali Ali Katolila" (Pengo) wameingia mkataba huo na Brainstormusic mwezi wa pili mwaka huu na tayari hivi sasa wameshapikwa vizuri na wanategemea kuachia single ya mpya chini ya usamimizi wa Label hiyo mwezi ujao.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wadananda waimeingia mkataba wa kurekodi album ya muziki, TV Shows, Filamu na Management kupitia "Brainstormusic". Hivi mpaka dakika hii tayari wameshakamilisha Photoshoots,Nyimbo yao mpya, na taratibu za kushoot video ndio zinaendelea.
Wadananda watakua wasanii wa pili baada ya CPwaa kuingia mkataba na label hiyo ambayo imedhamiria kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya burudani. Wasanii wengine ambao wapo kwenye hatua za mwisho za kupitishwa na label hiyo ni chipukizi wawili " Nurdin" na "Feisal". Tayari kampuni hiyo imeshaini kikundi kimoja cha ngoma za asili na kwa sasa hivi bado wanapitia maombi mengi ya wasanii wa Hip Hop na Bongeflava.
"...Tumepata maombi mengi sana na bado tunapokea maombi kutoka wasanii mbalimbali Tanzania.Wengi ni wasanii wa Hip Hop na tuko makini kuhakikisha tunafanya kazi na watu wanaojitambua,wamedhamiria,wanajituma na wana vipaji. CPwaa alishatoka na sasa hivi kinachofanyika nikumuweka vizuri kwenye ramani ya soko la kimataifa. Wadananda wameshapikwa wameiva na sasa ni zamu yao kutoka. Watu wategemee vitu vizuri kutoka kwao na Brainstormusic kwa ujumla. Kwa kuanzia tuu tunataka mwaka huu at least tuwe tumeshaini wasanii au makundi matano.".......ameongezea Talent Manager wa Brainstormusic "Almah Aboubakar Salum"
No comments:
Post a Comment