Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, wakati wa mwendelezo wa ziara hiyo ndani ya Mkoa wa Tabora.Kinana amemaliza ziara yake katika Wilaya ya Igunga na Nzega na leo kuhamia wilayani Uyui, katika suala zima la kuimarisha chama, kutekeleza na kuhimiza maendeleo ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010, sambamban na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuni kwa namna moja ama nyingine,zira hiyo itakuwa ni ya siku kumi ndani ya mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya Bukene, wilayani Nzega jana.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo cha utii wa chama hicho, baada ya kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega jana.
Katibu wa NEC,Itikadi,Siasa na Uenezi, Ndugu Nape Nnayue akiwahutubia wakazi wa Bukene, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, mkoani Tabora.
Kinana akishiriki kufyatua tofali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matofali wa akina mama wa CCM Wilaya ya Nzega. Mradi huo umefadhiliwa na Mbunge wa Viti MaalumMkoa wa Tabora, Munde Tambwe (pichani kushoto), katika eneo la Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega jana. Nyuma ni Mbunge wa jimbo la Nzenga,Dkt.Hamis Kingwangallah.
No comments:
Post a Comment