Private Brian Salvatory Rweyemamu
Bwana Salvatory Rweyemamu wa Kinondoni Dar es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake mpendwa Private Brian Salvatory Rweyemamu aliyefariki alfajiri ya kuamkia tarehe 15 Mei,2014 katika hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alipokuwa akitibiwa.
Mipango ya mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika Jumamosi inafanyika. Msiba uko nyumbani kwa Bwana Salvatory Rweyemamu Kinondoni jirani na Vijana Social Hall ama Mango Garden, jijini Dar es salaam. Ratiba ya mazishi itatolewa punde.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki walioko Dar es Salaam, Kagera, Malawi, Afrika Kusini, Uingereza na Canada.
Sisi tulimpenda, lakini Bwana kampenda zaidi.
Jina la Bwana na lihimidiwe.
Amin
Sisi tulimpenda, lakini Bwana kampenda zaidi.
Jina la Bwana na lihimidiwe.
Amin
No comments:
Post a Comment