Kundi la walemavu, wajasilimali wafanyabiashara ndogo ndongo, leo May 20, 2014 wamefunga makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru (Karume) kwa muda wa masaa matatu wakishinikiza Serikali iwapatie maeneo ya kufanyia biashara baada ya kuwaondoa katika eneo la Mtaa wa Kongo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa Juu ya gari kuangalia tukio hilo lililodumu kwa muda wa zaidi ya masaa matatu katika eneo la makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru (Karume).
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Baadhi ya Walemavu wakiwa wamekaa katikati ya Barabara.
Msururu mrefu wa Magari uliosababishwa na mgomo huo wa wafanya biashara ndogondogo na Walemavu.
Hapa hapiti mtu leo mpaka kieleweke........
Muuza maji ya kwenye vifuko akimuhudumia mteja wake.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa mchana wa leo. PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA MTAA KWA MTAA BLOG.
No comments:
Post a Comment