Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia, Brazil, jana
walijikuta wakionekana kama timu ya kata mbele ya Wajerumani
waliowaangusha mvua ya magoli katika mechi ya nusu fainali.
Mashabiki wa Brazil wakiwa na majonzi makubwa
Kwa
ushindi huo wa mabao 7-1 Ujerumani imeingia fainali na sasa inasubiri
mshindi kati ya Uholanzi na Argentina ili kufahamu itakayekutana naye.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Brazil walifungwa magoli matano katika kipindi cha kwanza na kuwaacha
mashabiki wa Brazil wasiamini macho yao. Hiyo ni aibu kubwa kwa timu ya
Brazil kuwahi kufungwa mabao mengi kiasi hicho tangu miaka 80
iliyopita.
“Kila kitu kilikuwa sawa mpaka pale tulipofungwa bao la
kwanza,” kocha wa Brazil Luis Scolari alisema. “Kisha, tukajichanganya
na baadaye tukaanza kupaniki na kasha kila kitu kikawa vizuri kwa
Brazil na kwetu kuwa hovyo.”










No comments:
Post a Comment