Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akielekeza jambo katika ukaguzi wake
Mkaguzi wa Tarafa ya Goima A.Insp Msika akisoma taarifa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Wananchi wa Tarafa ya Goima wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP
Kamanda MISIME kushoto akifuatiwa na OCD Chemba Vicent Chua - SSP, OC-CID Lutha na Mkaguzi wa Tarafa Yuda akiongea jambo katika tarafa ya Kwamtoro Wialayani Chemba Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akiongea na viongozi na wananchi wa tarafa ya Farkwa Wialaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma
Wananchi wa Tarafa ya Farkwa Wialaya ya Chemba Dodoma wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVI MISIME – SACP amewataka viongoz wa Tarafa za
Farkwa, Kwamtoro, Mondo na Goima Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kushirikiana na
Jeshi la Polisi kuielimisha jamii kuanzia ngazi ya familia kwa kuwaeleza kuwa
matatizo na migogoro iliyopo ndani ya jamii haitatuliwi kwa kujichukulia sheria
mikononi bali ni kwa kufanya majadiliano ndani ya vikao katika ngazi mablimbali
na kufikia mafanikio.
Aliyasema hayo Wilayani Chemba alipokuwa
akitembelea tarafa nne za Wilaya hiyo (Farkwa, Kwamtoro, Mondo na Goima ) ili
kuongea na viongozi wa tarafa hizo na kutoa elimu ya Polisi jamii pamoja na
kuwakabidhi rasmi wakaguzi wa tarafa na Polisi kata ili waweze kushirikiana nao
kutoa elimu kwa jamii juu ya utii wa sheria bila shuruti, kujenga familia
zisizokuwa na mhalifu na kubaini viini vya uhalifu, vurugu na migogoro katika
maeneo yao.
Kamanda MISIME amewaeleza maana ya Polisi
jamii kuwa ni ushirikishwaji wa kila mtu katika jamii kulingana na nafasi yake
ili kuleta amani, utulivu, usalama na ustawi wa jamii, hivyo jamii inapaswa
kushiriki katika suala la ulinzi na usalama.
Aidha Kamanda MISIME amesema viongozi
wanatakiwa kuimarisha kamati za ulinzi na usalama za tarafa, kata, vitongoji,
vijiji, mitaa na hata katika maeneo ya ibada lakini pia kuzitambua rasilimali
za kiuchumi, kuzilinda na kuheshimu mipaka ili kuweza kutatua kero za
mbalimbali za wananchi.
Pia aliongeza kwa kusema malengo makubwa ya
Polisi jamii ni kuweka mazingira ya ushirikiano wa dhati kati ya Polisi na wananchi
ili jamii ipate ujasiri iweze kukemea, kufichua, kuzuia uhalifu na kutatua
migogoro kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo pamoja na kujenga utayari wa
kuchukia uhalifu. Vilevile kuwa tayari kutoa ushahidi wa kile walichoona wakati
tukio la kiuhalifu lilipotokea.
Pamoja na hayo aliwapongeza wananchi kupitia
viongozi wa tarafa hizo kwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo
vimesaidia kupunguza uhalifu na aliwataka waendelee kuimarisha na kuunda
vikundi vingine vipya.
Nao viongozi mbalimbali wa tarafa hizo
wakiwemo Maafisa tarafa, Madiwani wa kata, Maafisa ugani, Watendaji wa kata na
tarafa, wenyekiti wa Serikali za mitaa, Viongozi wa dini, Wazee maarufu wa kata
na tarafa pamoja na viongozi wa vikundi vya ulinzi shirikishi wamemshukuru
Kamanda MISIME kwa kuweza kufika kwenye tarafa hizo na kuzungumza nao namna ya
kushirikisna na Polisi katika kuimarisha ulinzi ili kupunguza uhalifu katika
tarafa hizo na kusema kuwa elimu waliyoipata wataifanyia kazi kwa kuelimisha
jamii juu ya ulinzi na usalama katika jamii inayowazunguka.
Halikadhalika viongozi hao wamesema Polisi
jamii imewezesha wananchi wakawa na mafunzo mazuri ya kuepuka mambo maovu pia
wameomba Jeshi Polisi Mkoa wa Dodoma liendelee na utaratibu huu wa kutembelea
kata na tarafa ili kuweza kutoa elimu itakayowapatia mbinu mbalimbali za kuweza
kukabiliana na uhalifu na wahalifu.
Wameliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
liendelee na utaratibu wa kuwapatia mafunzo ya udereva vijana wao wanaoendesha
pikipiki (bodaboda) ikiwa na pamoja na kuwapatia leseni za udereva ili kuepusha
ajali zitokanazo na kutojua sheria za usalama barabarani.
Katika kuhitimisha vikao hivyo na viongozi hao
wa tarafa na kata Kamanda MISIME amesema viongozi wa ngazi zote na wananchi
wajijengee utamaduni wa kuitisha vikao vya pamoja na kujadili namna ya kubaini
viashiria vya uhalifu na migogoro katika
maeneo yao.
Pia aliwataka kuzingatia daftari la wakazi ili
kuweza kuwajua wakazi wa maeneo yao na kuwatambua wageni na wavamizi ambao wakati
mwingine ndiyo chanzo cha migogogo na uhalifu.









No comments:
Post a Comment