Waziri wa
ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa iramba katika jimbo la mwibara kabla ya kuzindua
kivuko cha mv. mara chenye uwezo wa kubeba tani
25 yani magari manne na abiria 50
Waziri wa
ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa kivuko kipya cha MV Mara kitakachotoa huduma kati ya maeneo ya iramba bunda na majita musoma
vijijini. kutoka kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Mara Mhandisi Evarist Ndikilo
akifatiwa na mbunge wa jimbo la Mwibara Alphaxad Kangi Lugora, wengine kutoka
kulia ni katibu mkuu wa wizara ya ujenzi mhandishi Mussa Iyombe akifatiwa na
mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono pamoja na mwenyekiti wa CCM mkoa wa mara
Christopher Sanya.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waziri wa
ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe cha kivuko cha MV Mara
kuashiria kukizindua rasmi kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya maeneo ya Iramba
na Majita katika wilaya mbili za Bunda na Musoma vijijini
Waziri wa
ujenzi, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wakazi wa Mwibara mara baada ya
kufungua kivuko cha MV Mara
Picha ya kivuko kipya cha MV Mara kama
kinavyoonekana katika picha kabla ya kufunguliwa
Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
zawadi za kimila kutoka kwa wenyeji wa bunda za kumtambua kuwa mkazi wa mji huo
kwa kimila.
Waziri wa
ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa katibu mkuu wa wizara
ya ujenzi mhandisi mussa iyombe kushoto huku mwenyekiti wa bodi ya Temesa
Herbert Mrango pamoja na mtendaji mkuu wa Temesa mama Marcelina Magessa
wakisikiliza kwa makini
Waziri wa
ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia na wanachama wapya wa chama cha
mapinduzi (CCM) walioamua kujiunga na chama hicho mara baada ya waziri magufuli
kumaliza kuhutubia mkutano.
Waziri wa
ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mwenyekiti wa bodi ya Temesa
balozi Herbert Mrango huku mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono aliyessimama
kulia na mbunge wa Mwibara Kangi Lugora wakwaanza kushoto wakiangalia
Baadhi ya wakazi wa Iramba katika jimbo la Mwibara
wakiwa wamepanda juu ya miti ili kumshuhudia Waziri wa ujenzi Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya uzinduzi wa
kivuko hicho
Picha ya boti ambayo ilikuwa ikitumika awali
kuvusha watu kati ya Majita na Iramba
kwa gharama ya shilingi 2000/=














No comments:
Post a Comment