Ukitaka
kufanya biashara yoyote ile unatakiwa kufanya utafiti. Kutokufanya utafiti ni
chanzo cha biashara nyingi kuharibika. Lazima ujiulize kwamba unataka kufanya
biashara gani? Usiseme unataka kufanya biashara yoyote ile kwani kusema kwamba
unataka kufanya biashara yoyote ile ni kupoteza mwelekeo kwa kuwa utakuwa hujui
unataka kufanya nini. Kama hujui cha kufanya hakuna kitu utakachokifanya. Hili
ni tatizo la watu wengi. Hata baadhi ya watu niliokutana nao wakitaka ushauri
wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili. Njia ya kukusaidia kuamua ufanye
biashara gani ni kwa kujiuliza umewahi kufanya kazi au biashara gani? Umesomea
nini? Vipaji vyako ni vipi? Ni biashara ipi au kazi ipi unapenda zaidi kuliko
nyingine na kwa sababu gani? Ukisha jiuliza maswali haya chukua kalamu na
karatasi uandike maswali yako na kuyajibu. Ukikagua maswali na majibu yako
utagundua shughuli unayoipenda, unayoiweza na una kipaji nayo na hiyo ndiyo
inayokufaa. Ukishachagua biashara unayoipenda ni rahisi sana kufanikiwa kwani
shughuli utazifanya kwa hiyari bila kujilazimisha. Kama unashindwa kuamua ni
biashara gani ufanye, soma sura ya sita katika kitabu hiki. Nimeelezea kuhusu
mawazo yanayoweza kukusaidia kuanzisha biashara mbalimbali ambazo unaweza
kuzifanya. Kama utakuwa bado hujafikia uamuzi baada ya hapo basi tafuta na
wasiliana na washauri ili mbadilishane mawazo na ufundishwe jinsi ya kuamua
ufanye biashara gani.
Mambo mengine unayotakiwa kuyafanyia utafiti ni:-
(i) Kujua siri ya bishara unayotaka kufanya ili upate mbinu za kupata mafanikio. Unaweza kupata siri au kujifunza mbinu kutoka kwa watu wanaofanya biashara kama unayotaka kufanya. Suala hili ni gumu sana kwani wafanyabiashara wengi huwa wanaficha siri za biashara zao ili kulinda wasizidiwe maarifa na washindani wao. Unaweza kuipata siri hiyo kama utakwenda kupata ushauri toka kwa mfanyabiashara ambaye yuko mbali na mahali unapofanyia biashara, au tafuta ushauri kwa wataalamu wa mambo ya biashara.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
(i) Kujua siri ya bishara unayotaka kufanya ili upate mbinu za kupata mafanikio. Unaweza kupata siri au kujifunza mbinu kutoka kwa watu wanaofanya biashara kama unayotaka kufanya. Suala hili ni gumu sana kwani wafanyabiashara wengi huwa wanaficha siri za biashara zao ili kulinda wasizidiwe maarifa na washindani wao. Unaweza kuipata siri hiyo kama utakwenda kupata ushauri toka kwa mfanyabiashara ambaye yuko mbali na mahali unapofanyia biashara, au tafuta ushauri kwa wataalamu wa mambo ya biashara.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
(ii) Fanya utafiti wa soko la bidhaa unazouza au
unazotarajia kuuza. Jiulize, je bidhaa unazotaka kuziuza zina soko? Utawauzia
watu gani na utauzaje? Kama wewe ni mzalishaji, una mazao / bidhaa unapaswa
kuuza kwa jumla, mchanganyiko ama rejareja? Je utatangaza vipi bidhaa zako?
Maelezo ya namna ya kutangaza bidhaa zako utayapata katika Sehemu ya Tatu ya
Kitabu hiki. Utafiti wa soko unaweza kuufanya kwa kuwauliza wafanya biashara
waliotangulia maswali hayo ya utafiti kwani wao wamekuwapo kwenye soko na
wanazijua siri za soko.
(iii) Tengeneza bajeti yako kwa kuorodhesha vitu
vinavyohitajika na gharama zake ili kuweza kuanzisha biashara yako. Vitu hivyo
ni:-
(a) Gharama za Kujenga au kupanga ofisi
(b) Gharama za Leseni ya biashara
(c) Makadirio ya kodi toka TRA
(d) Garama ya vifaa vya ofisi yaani, Samani, makaratasi, mitambo, mashine, nk
(e) Manunuzi ya malighafi au bidhaa za kuanzia biashara
(f) Idadi ya wafanyakazi na gharama za mishahara yao.
(g) Gharama nyinginezo kama vile, umeme, maji, nk.
(a) Gharama za Kujenga au kupanga ofisi
(b) Gharama za Leseni ya biashara
(c) Makadirio ya kodi toka TRA
(d) Garama ya vifaa vya ofisi yaani, Samani, makaratasi, mitambo, mashine, nk
(e) Manunuzi ya malighafi au bidhaa za kuanzia biashara
(f) Idadi ya wafanyakazi na gharama za mishahara yao.
(g) Gharama nyinginezo kama vile, umeme, maji, nk.
(iv) Unatakiwa kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara yako. Mtaji huo utaujua baada ya kujumlisha gharama zilizoorodheshwa katika kupengele namba (iii)Gharama hizi ni za mwaka ule wa kwanza wa kuanzia
(v) Tafuta Mtaji. Mtaji unaweza kupatikana kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo:-
(a) Akiba au mshahara
(b) Msaada au mkopo kutoka kwa ndugu na jamaa.
(c) Kuingia ubia na mtu mwenye mtaji
(d) Mkopo toka baadhi ya asasi kama vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), NGO za kifedha sipokuwa Benki kwani hizi huwa hazitoi mikopo kwa mtu anayeanzisha biashara.
TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA BIASHARA
(a) Akiba au mshahara
(b) Msaada au mkopo kutoka kwa ndugu na jamaa.
(c) Kuingia ubia na mtu mwenye mtaji
(d) Mkopo toka baadhi ya asasi kama vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), NGO za kifedha sipokuwa Benki kwani hizi huwa hazitoi mikopo kwa mtu anayeanzisha biashara.
TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA BIASHARA
Baada ya
kufanya utafiti na kupanga mipango ya kuanzisha biashara unatakiwa kwanza
kuangalia taratibu za kisheria ambazo unatakiwa kuzifuata na kuzitekeleza. Kama
biashara yako ni ndogo anza kama mtu binafsi. Faida ya kuanza biashara kama mtu
binafsi ni urahisi wa kuanzisha biashara; urahisi na wepesi wa kutoa maamuzi
kwani huhitaji ridhaa ya mtu mwingine kabla ya kutoa uamuzi; mtaji unaohitajika
utakuwa mdogo kutokana na gharama za uendeshaji kuwa ndogo, biashara hii
inaweza kuendeshwa kwa msaada wa familia kwa kumtumia mke au mume, watoto au
ndugu na jamaa na raslimali za familia kama nyumba na samani. Unapoanzisha
biashara na kuiendesha mwenyewe unakuwa huru tofauti na mifumo mingine.
Matatizo ya kufanya biashara kama mtu binafsi ni:-
Kushindwa kupanua biashara
yako kwa ufinyu wa mtaji; kufilisiwa mali zako za binafsi iwapo biashara yako
itafilisika kwani katika mfumo huu mali ya biashara na mali binafsi si rahisi
kuzitenganisha; Kuongeza mtaji inakuwa ni vigumu, hivyo unaweza kushindwa
kupanua biashara yako. Ili kuepukana na matatizo niliyoyataja hapo juu unaweza
kuungana na watu wengine kufanya biashara kwa ubia. Faida za kufanya biashara
kwa ubia ni: Kupata fursa ya kuongeza mtaji kwa kushirikiana na wafanyabiashara
wengine ambao wataleta mitaji yao; Kuongeza ujuzi katika shughuli kwa kuleta
wataalamu pale taaluma Fulani inapohitajika. Matatizo ya kuendesha biashara kwa
njia ya ubia ni: Kufilisiwa mali zako binafsi endapo biashara yako itafilisika;
kudhulumiana mali endapo moja wa wabia atakuwa si mwaminifu ambapo anaweza
kuingia mikataba mibovu na kusababisha hasara ambayo itabebwa na wabia wote.
Ni
muhimu kuwachunguza watu tunaotaka kujiunga nao ili tujue kama ni waaminifu.
Pia ni vyema kuwapo na mkataba wa maandishi mnapoanzisha biashara ya ubia
mkimshirikisha mwanasheria kama shahidi ili kujikinga na kudhulumiana; Kufariki
kwa mbia mmoja kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia; kotokuelewana kwa wabia
kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia. Kama biashara ikikua unaweza kuanzisha
kampuni.
Mfumo wa uendeshaji wa kampuni unazo faida zifuatazo: unatenganisha
majukumu ya wamiliki mali na kampuni yaani kampuni inaposajiliwa inakuwa
inakuwa na hadhi na kutambulika kisheria kama ni mfumo tofauti na wamiliki.
Mfumo huu unatenganisha majukumu kati ya menejimenti na wamiliki wa kampuni;
madeni ya kampuni yatalipwa hadi kufikia kikomo cha mtaji uliowekezwa na
wamiliki. Hivyo, mali binafsi za wamiliki wa kampuni haziwezi kukamatwa kufidia
madeni ya kampuni endapo kampuni itafilisika. Mfumo wa kampuni unatoa nafasi ya
kupanua mtaji kwa kukusanya mitaji kwa kuongeza wanahisa au kupitia soko la
mitaji ya hisa. Mfumo huu ndiyo unafaa kwa biashara kubwa kwani unatoa nafasi
ya kupanuka kwa biashara na kuendelea kuwapo kwa biashara hata kama baadhi ya
wamiliki wake wakifa au kujitoa katika kampuni.
Mambo ya muhimu ya kutekeleza kisheria kabla ya kuanzisha biashara ni:-
(a) Kuwa na
ofisi
(b) Kukata
leseni
(c)
Kusajiliwa na TRA kama mlipokodi na kupewa namba ya mlipakodi
(d)
Kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato ya awali
(e)
Kutimiza masharti mengine ya keshiria kuwa mfano kama wewe unataka kufanya
biashara ya ukandarasi wa ujenzi wa majengo lazima usajiliwe kwenye Bodi ya
Wakandarasi.
Kama unafanya
biashara ya kati au kubwa unapaswa kufuata sheria. Ni makosa kufanya biashara
bila kufuata sheria za nchi. Hata hivyo, kuna biashara zingine ndogo ndogo sana
kiasi kwamba uanzishaji wake si rahisi kufuata sheria hizo hapo juu, mfano
uuzaji wa maandazi, karanga na vitu vingine vidogovidogo. Hizi zinaitwa
biashara zisizo rasmi au biashara ndogondogo. Ni vyema ukachunguza kama
biashara unayoifanya ni ndogo au kubwa ili ujue kama unapaswa kufuata taratibu
za kisheria au la, kwani kutokujua utaratibu na sheria siyo kinga ya kukufanya
usishitakiwe.
No comments:
Post a Comment