HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAULID KITENGE WA RADIO ONE AHAMIA RADIO EFM


Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela.
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo.

Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: