Naamini ni wengi wanaomiliki simu za kisasa ‘smartphones’ ambazo zinaendana na teknolojia ya sasa iliyozidi kurahisisha maisha ya mwanadamu kupitia simu hiyo ya kiganjani. Lakini yawezekana si wote ambao wanaifahamu ‘smartphone’ ya kwanza kuingia sokoni.
Smartphone ni nini?
Ni simu ya mkononi ambayo inauwezo wa kufanya mambo mengi yanayofanywa na kompyuta.
Smartphone ya kwanza
IBM Simon ndio ilikuwa ‘Smartphone’ ya kwanza duniani iliyoenda sokoni Agosti 16, 1994 na leo Agosti 16, 2014 inatimiza miaka 20.
Hata hivyo IBM Simon ilikuwa haiitwi ‘Smartphone’ kipindi hicho, lakini ilikuwa na ‘features’ nyingi zilizoko kwenye ‘Smartphone’ za sasa.
“But it had a lot of the features we see today. It had a calendar, it could take notes and send emails and messages and combined all of this with a cell phone.” amesema Charlotte Connelly ambaye ni content developer wa makumbusho ya sayansi ya London.
IBM Simon ilikuwa na uzito wa gram 500.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
“It looks like a grey block but it’s not as big as you’d imagine, It had a stylus and a green LCD screen, which is similar in size to the iPhone 4. In fact, it’s not a bad looking thing.” Aliongeza ms Connelly.
Charlotte Connelly, content developer wa makumbusho ya sayansi ya London.
Hata hivyo inasemekana ukubwa wa bei (kwa wakati huo) pamoja na maisha mafupi ya betri ni miongoni mwa sababu za kupotea haraka kwa simu hizo sokoni ndani ya miaka miwili baada ya kuzinduliwa.
IBM Simon ilikuwa ikiuzwa $899, na hapakuwa na internet ya simu wakati huo hivyo haikufanya vizuri. Ziliuzwa simu 50,000 tu na nyingi zilinunuliwa na wafanyabiashara.
Motorola ya 1984 (kushoto), IBM Simon ya 1994 (katikati) na simu za sasa 2014 (kulia)
Katika kuadhimisha miaka 20 ya IBM Simon, Makumbusho ya sayansi ya London, wataiweka simu hiyo kama sehemu ya maonesho ya ‘Information Age’ mwezi Octoba mwaka huu.
IBM Simon ilitengenezwa na kampuni ya IBM pamoja na kampuni ya simu ya Marekani, BellSouth.
IBM wamesema waliita Simon kwasababu ilikuwa simple na iliweza kufanya karibu kitu chochote mtu alichohitaji.
Source: BBC, Daily Mail
-
No comments:
Post a Comment