Kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za upendeleo katika utoaji nafasi za ajira 200 kwa watu waliyoomba nafasi hizo kupitia idara ya uhamiaji imebaini kuwa nafasi hizo zimetolewa kwa upendeleo bila ya kufuatwa taratibu, kanuni na sheria ya utoaji wa ajira hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil amesema kamati hiyo imeweza kubaini kuwa mambo mengi yalifanywa kiujuma jumla sana na hivyo kutoa mwanya wa watu kupindisha mambo.
Kamati hiyo iliundwa Agosti Mosi mwaka huu, chini ya watu watano ikiongozwa na yeye mwenyewe katibu mkuu wa wizara ya hiyo.
Iadha katika mkutano huo jeshi la polisi kupitia mkurugenzi wa makosa ya jinai kamanda Isaya Mngulu amesema jeshi hilo litafanya operesheni ya kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wakiwemo waganga wa kienyeji wanaojihusisha na vitendo vya kuwaua ama kuwajeruhi walemavu wa ngozi kwa imani zao za kishirikina.
CHANZO: ITV TANZANIA
No comments:
Post a Comment