Baadhi ya wapenzi na wanachama wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakishangilia baada ya gari lililokuwa
limembeba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alipowasili leo Makao Makuu wa
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, kwa mahojiano. (Picha zote na Joseph
Senga)
Mbowe akitoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi baada ya kuhojiwa wa saa 5.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mawakili wawili kati ya watano, Mabere Marando
(kushoto) na Profesa Abdallah Safari, wakiwasili katika Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi jijini Dar es Salaam, ambako Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila
akihojiwa na askari Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es
Salaam kwa kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.
Mmoja wa wanachama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), ambaye jina lake halikuweza kupatikana, akipewa kibano na
askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), nje ya Makao Makuu ya Polisi, Dar
es Salaam.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakimpa
kichapo mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango, nje
ya Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam.
Askari wa Kikosi cha Mbwa, wakiranda na mbwa wao nje
ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, kuwatawanya wananchi na
waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment