Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kuwa na watoto kunaweza kukufanya ujitume zaidi kazini, na hiyo huwatokea zaidi wanawake.
Utafiti unadai kuwa kuwa na mtoto zaidi ya mmoja kunaweza kumfanya mtu awe mzuri maradufu kazini. Ilibainika kuwa akinamama wenye watoto walau watatu hufanya vizuri zaidi.
Watafiti wa Federal Reserve Bank ya St. Louis, Missouri, Marekani waliwafanyia utafiti takriban wanaume na wanawake 10,000. Walikuwa wakichunguza ile imani kuwa kuwa na watoto wengi humfanya mtu asijitume.
Na matokeo yalionesha kuwa wanaume wenye mtoto mmoja walikuwa wakifanya kazi sawa au chini ya wenzao wasiokuwa na watoto. Wanaume wenye mtoto zaidi ya mmoja hata hivyo walikuwa productive zaidi ya wale wenye mmoja ama wasiokuwa naye kabisa.
Kwa wanawake, wale wasiokuwa na watoto walionekana kuwa nyuma ya wale wenye watoto ambao hujituma muda wote wa maisha yao ya kazi.
No comments:
Post a Comment