Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Johnson Lukaza
Na Happiness
Katabazi (UB)
HATIMAYE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdomo wake Mwesiga Lukaza
waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika Akaunti ya
Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia Katika Kesi
iliyokuwa ikimkabili.
Hukumu hiyo
Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu
Mkazi Pamela Mazengo.
Lukaza ambaye
pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na
Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex
Mshumbusi.
Akisoma
hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama
imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali, Mahakama
yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote Wawili kwasababu
upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao ungeishawishi
Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao.
No comments:
Post a Comment