Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka.
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
NA CHALILA KIBUDA
WAZIRI wa Ardhi,
Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibajuka amesema kuwa hawezi kujiuzulu katika
nafasi ya uwaziri kutokana fedha ya
Tegeta ESCROW.
Akizungumza na
Waandishi na Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat
Regency,Anna alisema kuwa udalali wake fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi
katika shule za Taasisi ya Johansson Girls Education Trust.
Alisema fedha hiyo aliyoipata ni ni bil 1.66 ambazo zilitoka
katika kampuni ya James Rugemalira ni kwa ajili ya msaada wa shule za Taasisi ya Johansson
Girls Education Trust .
Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi
ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James Rugemalira
ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi. ‘’Nikijiuzulu hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani
fedha nilizopata ni za shule na kwa ajili kukomboa elimu nchini hasa kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za shule’’alisema Anna.
Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai
hata Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP
,Reginard Mengi alitoa sh.milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.
Anna alisema kuwa
wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi
kufanya hivyo na kama angetaka fedha hiyo angeweza kufuata hata katika shule na
kuchukua.
CHANZO: MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment