Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu mwenezi wa Chadema, Kata ya Rigicha wilayani hapa, Bahati
Mayala (37) amelazwa katika Hospitali Teule ya Nyerere baada ya kujeruhiwa kwa
mshale wakati akitoka kwenye kampeni.
Tukio hilo
lililotokea Desemba 5, aa 1:30 jioni katika Kijiji cha Kitembele
limethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali hiyo. Mganga mkuu wa
hospitali hiyo, Calvin Mwasha alikiri kupokewa kwa majeruhi akiwa na mshale mgongoni
saa 6:00 usiku juzi na kufanyiwa upasuaji kutoa silaha hiyo ya jadi.
Mwasha alisema mshale huo ulikuwa umeingia inchi sita katika
eneo la mapafu. Akizungumza na gazeti hili hospitalini hapo, Mayala alisema
alipigwa baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa.
“Nikiwa njiani katika Kitongoji cha Ngayani ghafla nikasikia kitu
kinakita mgongoni...nikaona watu wawili wanakimbia ambao niliwafahamu kwa nguo
walizokuwa wamevaa na majina, wote wa Kijiji cha Kitembele. Niliposhika
mgongoni nikakuta mshale, nikapiga kelele kuomba msaada,” alisema.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Alisema wananchi walikusanyika na kumpeleka kituo cha afya cha
Natta, lakini walishindwa na kumpa rufaa kwenda hospitali hiyo. Kuhusu chanzo
cha tukio, alisema ni kutokana na masuala ya kisiasa kwa kuwa siku hiyo kwenye
mkutano wao kulitokea vurugu zilizosababishwa na wafuasi wa vyama vingine na
wakati anarudi nyumbani akashambuliwa.
Kamanda wa polisi wa Wilaya ya Serengeti, Pius Mboko alikanusha
madai ya kuhusisha siasa, akisema Mayala alijeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa
wezi wa ng’ombe. “Si suala la siasa bali alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa
wanafuatilia wezi wa mifugo, ndipo akapigwa mshale wakati akiwa na watu
wengine,” alisema.
“Watuhumiwa hawajakamatwa na tunaendelea kufuatilia,” alisema
bila kubainisha ni ng’ombe wangapi walikuwa wameibwa na walikuwa ni mali ya nani. Alisema
ng’ombe hao waliibwa katika Kijiji cha Monuna.
No comments:
Post a Comment