MNENGUAJI WA BENDI YA TWANGA PEPETA AISHA MADINDA KUZIKWA KESHO IJUMAA JIJINI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Aisha Madinda - enzi za uhai wake alipokuwa stejini.
Aliyekuwa mnenguaji na mwimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda aliyefariki jana asubuhi, atazikwa siku ya kesho Ijumaa mchana badala ya leo Alhamis kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Mtoto wa kwanza marehemu, Feisal amesema kuwa polisi wamesema ni lazima mwili wa mama yake ufanyiwe upasuaji (postmortem) ili kujua chanzo cha kifo chake.
Awali ndugu wa marehemu walisema hawahitaji Asha Madinda afanyiwe upasuaji, lakini baada ya polisi kutembelea eneo la tukio la kifo chake huko Mabibo, wamesema ni lazima upasuaji ufanyike.
Feisal amesema upasuaji unatarajiwa kufanyika leo mchana hali inayowalazimisha kubadili ratiba ya mazishi. Aisha Madinda sasa atazikwa kesho mchana baada ya sala ya Ijumaa.
CHANZO: GPL

No comments

Powered by Blogger.