HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » SHIRIKA LA RELI LIMEPOKEA MABEHEWA 50 YA MIZIGO NA 22 YA ABIRIA.

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Serikali imepokea mabehewa 50 ya mizigo na mabehewa 22 ya kisasa ya abiria ikiwa ni sehemu ya mabehewa 274 yanayotawarajiwa kuwasili nchni ili kuboresha huduma za usafiri wa mizigo na abiria hapa Nchni.
 Akizungumza na waandishi wa habari, waziri wa uchukuzi Daktari Harrison Mwakyembe amesema kuingia kwa mabehewa hayo ni ishara ya jitihada za serikali katika kuimarisha huduma ya usafiri wa reli ambapo amesema amesisitiza serikali imetumia zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha sekta ya reli nchni.
 
 Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli nchni Bwana Kipalo Kisamvu amesema mabehewa hayo ya abiria ni kwa ajili ya safari katika mikoa ya mwanza  na kigoma, na kusisitiza shirika hilo la Reli kwa kushirikiana na wakala wa usafiri wa majini na nchi kavu wako katika mchakato wa kuanzisha usafiri wa haraka wa abiria ambao utasimama katika vituo vikubwa pekee. (Picha na Ernest Nyambo)

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: