WAZIRI SIMBA AFUNGUA KONGAMANO LA KUOMBEA TAIFA (SHILO) KANISA LA ASEMBLIESS OF GOD LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


 Askofu Mkuu wa Kanisa la Asembliess of God la Mlima wa Moto la Mikocheni, Getrude Lwakatare akizungumza na wanahabari.
 Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) na Askofu Mkuu wa Kanisa la Asembliess of God la Mlima wa Moto la Mikocheni, Getrude Lwakatare (kulia),  pamoja na Askofu  Danstan  Maboya kutoka Arusha wakishangilia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kuliombea Taifa la kufunga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2014 liitwalo Shilo lililoandaliwa na kanisa hilo Dar es Salaam jana
 Wakinana wenye sare maalumu wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
 Hapa ni burudani tu kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku.
Askofu mama Lwakatare akiombewa.
 Wachungaji wakimuombea Waziri Simba.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Asembliess of God la Mlima wa Moto la Mikocheni, Getrude Lwakatare akizungumza na wanahabari.

Waumini wakiwa kanisani.
Kanisa likiwa limejaa. Hakika inapendeza mbele ya mungu.
Waumini waliojumuika katika tukio hilo.
Hapa ni kujinyenyekeza kwa mungu wakati wa maombi.
Viongozi wa kanisa wakiwa katika ibada hiyo 
Muumini wa kanisa hilo akisali kwa hisia kali 'kweli tumuache mungu aitwe mungu haleluya'
Viongozi mbalimbali wakiwa kanisani hapo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye ufunguzi huo wa Shilo.
Ni furaha tu na mikono juu katika uzinduzi huo.
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Bahati Bukuku na vijana wake wakitoa burudani.
Hapa ni burudani kwa kusonga mbele.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Askofu Danstan  Maboya kutoka Arusha, akizungumza katika uzinduzi huo wa Shilo..
Maombi yakiendelea

Dotto Mwaibale

TANZANIA haitaweza kuingia kwenye vita kutokana na amani iliyopo kutokana na maombi yanayofanywa na waumini wa dini mbalimbali nchini.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba wakati akifungua kongamano la kuliombea Taifa la kufunga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2014 liitwalo Shilo lililoandaliwa na Kanisa la Asembliess of God la Mlima wa Moto la Mikocheni linaloongozwa na Askofu Getrude Lwakatarae Dar es Salaam leo.

"Kutokana na maombi yanayofanywa na dini zote kamwe hatutegemei nchi yetu kuingia katika vita hilo halitakuja kutokea na hatulitegemei" alisema Simba

Simba alisema kuna kazi kubwa inayofanywa na watu wa mungu kila siku kuliombea taifa ndio maana Tanzania imekuwa na amani na utulivu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuilinda na kuitunza amani hiyo.

Askofu wa kanisa hilo, Dk. Getrude Lwakatare alisema ni utaratibu wa kanisa hilo kila mwishoni mwa mwaka kuliombea taifa ili nchi kuwa na amani na watu wake wawe na maendeleo.

"Kongamano la namna hii ufanyika kila mwaka na kunakuwepo na maombi mbalimbali" alisema Lwakatare.

Baadhi ya viongozi watakao shiriki kutoa mada katika kongamano hilo ni Askofu Philemon Tibananaso wa Kanisa la Pentecosti, Eugene Mrisa kutoka New Life Ministry na Danstan  Maboya kutoka Arusha. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments

Powered by Blogger.